Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi akitoa maagizo kwa TAKUKURU kuhusu kampuni ya Mwenga Hydro iliyopo katika wilaya ya Mufindi
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
MAMLAKA
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Iringa imeagizwa kuichunguza
kampuni binafsi ya usambazaji wa Umeme ya Mwenga hydro power ya wilayani
Mufindi kutokana na uwepo wa Taarifa za kutoza wananchi gharama zaidi ya Elfu
50 hadi 180 tofauti na bei elekezi ya shirilingi elfu 27 ili kuingiziwa Umeme.
Agizo
hilo limtolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi wakai wa ziara yake ya
Iringa mpya awamu ya pili Katika Tarafa ya Kibengu yenye lengo la kukagua
miradi ya Maji inayotekelezwa na serikali,
Mkuu huyo wa Mkoa akabaini kuwepo wa vitendo hivyo vya ongezeko la gharama za
kuingiziwa umeme na kuiagiza (TAKUKURU) kufanya Uchunguzi na kuchukua hatua.
Hapi alisema
kuwa hairuhusiwi kwa mwananchi yeyeto yule kuingiza nishati ya umeme kwa zaidi
ya elfu 27,000 kwa kuwa ndio maagizo ya serikali na wizara husika hivyo hiyo
habari ya wananchi kulipa kiasi kikubwa kuingiza umeme.
“Takukuru
anzeni mara moja kuichunguza kampuni hiyo ya Mwenga Hidro mara moja kwa kupitia
nyaraka zote muhimu ili kubaini nini kinaendelea huko” alisema Hapi
Hapi
akahoji maelekezo yanayompa mamlaka ya Mwekezaji huyo kutoza Zaidi ya bei za
serikali ametoa wapi hiyo mamlaka kwa kuwa serikali haijatangaza kuwa bei ya
kuingiza nishati ya umeme kwa wananchi kwa ajili ya maendeleo.
“Serikali
imepanga bei elekezi nchi nzima hivyo hata mkoani kwangu sihitaji kusikia kitu
kama hicho na takukuru mkibaini wamefanya makosa kamata weka ndani wote ambao
wanausika na hujuma hiyo” alisema
Na haya ndiyo majibu ya Meneja Uendeshaji wa
Kampuni hiyo Lydia Emmanuel akaeleza juu ya namna wanavyofanya kazi ya
usambazaji wa umeme vijijini nje ya wakala wa Usambazaji Umeme vijijini REA.
Kwa upande
wake meneja uzalishaji wa kampuni ya Mwenga Hidro Lydia Emmanuel alisema kuwa
wamepewa vijiji 32 kwa ajili ya kuingiza umeme kwenye vijiji hivyo lakini bado
kampuni hiyo inamamlaka ya kujipangia bei kwa kuwa ni kampuni binafsi.
“Kampuni
yetu ilipewa leseni ya kuingiza umeme mwaka 2011 katika maeneo ambayo TANESCO
haifanyi kazi hivyo kampuni hiyo imekuwa imekuwa inafanya kazi toka mwaka huo
hadi leo kwa gharama hizo” alisema
Naye kaimu
meneja wa Shirika la Umeme TANESCO Wilaya ya Mufindi Pascal Nayo, alisema kuwa
serikali ya awamu ya tano na zilizopita zilipita ziliagiza kuwa wananchi wote
wanatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 27000 tu.
Katika ziara hiyo wito umetolewa kwa wananchi
kutunza vyanzo vya maji ili kufanya upatikanaji wa maji kuwa endelevu katika
maeneo yao hiyo ni kutokana na wadau wa Maendeleo kuwekeza miradi ya maji
katika maeneo yao
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇