LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 28, 2020

RAIS DK. MAGUFULI AKAGUA LEO UJENZI WA MSIKITI UTAKAOKUWA MKUBWA KULIKO YOTE TANZANIA

Rais Dk John Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wakati akikagua Ujenzi wa Msikiti wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo



Ikulu Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambao utakuwa mkubwa kuliko misikiti yote nchini.

Msikiti huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya kuombwa na Rais Magufuli alipofanya ziara rasmi hapa nchini Oktoba 2016.

Akiongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally, Rais Magufuli ameona kazi za ukamilishaji wa jengo jipya la Msikiti na jengo la ofisi ya Taasisi ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco zikiendelea kukamilishwa, na ameelezea kufurahishwa kwake na ubora na uzuri wa Msikiti huo.


Rais Magufuli amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa kutekeleza ombi alilomuomba la kuwajengea Waislamu Msikiti mkubwa kuliko yote hapa nchini, na amempongeza Mufti wa Tanzania na Waislamu wote kwa kujengewa nyumba nzuri ya Ibada.


Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwajali Waislamu na kuwaombea msaada wa kujengewa Msikiti huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 97.


Akiwa na viongozi wenzake wa BAKWATA, Sheikh Mkuu Aboubakar Zubeir bin Ally ameongoza Dua ya kumuombea Mhe. Rais Magufuli na kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aiepushe Tanzania dhidi ya maradhi ya homa ya virusi vya corona, kudumisha amani na utulivu na kuombea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu ufanyike vizuri na kwa amani.
Muonekano wa Msikiti ambao Rais Dk. John Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ametembelea na  kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti huo wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa  Februari 28, 2020

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages