LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 4, 2020

RAIS WA PILI WA KENYA DANIEL ARAP MOI AMEFARIKI DUNIA LEO AKIWA NA UMRI WA MIAKA 96

NA BASHIR NKOROMO
RAIS mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi (pichani), ambaye alikuwa Rais wa Pili wa nchi hiyo, amefariki dunia leo asubuhi, Jumanne Februari 4, 2020, akiwa na umri wa miaka 96.

Rais wa sasa wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kifo hicho akisema, Mzee Moi amefariki katika Hospitali ya Nairobi ambako alikuwa akipatiwa matibabu na taarifa zinasema amekuwa akilazwa katika Hospitali hiyo tangu mwaka jana.


Taarifa zinasema, Msaidizi wa kibinafsi wa Mzee Moi, Lee Njiru pia amethibitisha kuwa Rais huyo wa pili wa Kenya ameaga dunia na Rais Kenyatta anatarajiwa kutoa taarifa kamili baadaye kuhusu habari hiyo.


Moi alikuwa rais wa Kenya kwa kipindi cha miaka 24 kabla ya kuacha madaraka mnamo 2002 baada ya Wakenya kumchagua kwa kura nyingi Mwai Kibaki aliyechukua nafasi yake.


Daniel Arap Moi aliingia madarakani mwaka 1978 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages