Tume ya taifa ya afya nchini China imesema watu 64 wamefariki jana Jumatatu katika jimbo la kati la Hubei, sehemu ambayo ugonjwa huo ulianzia, na kufikisha idadi jumla ya watu waliofariki kuwa 425.
Maafisa mjini Hong Kong wameripoti kifo cha kwanza kutokana na virusi vya corona katika jimbo hilo lenye utawala wake wa ndani.
Mtu huyo alisafiri kwenda Hubei Januari na amekuwa mgonjwa, kwa mujibu wa gazeti la South China Morning Post.
Taiwan imetangaza leo kuwa itawazuwia kuingia raia wote wa kigeni ambao wamekwenda China katika muda wa siku 14 zilizopita. Hatua hiyo haihusu raia wa China na Hong Kong na Macau.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇