LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 2, 2020

RAIS MAGUFULI KUAPISHA WAPYA KESHO

Ikulu, Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli kesho tarehe 03 Februari, 2020 atawaapisha viongozi wa Wizara, Mahakama, Majeshi na Mikoa aliowateua juzi kushika nyadhifa mbalimbali.

Viongozi watakaoapishwa ni Makatibu Wakuu 5, Naibu Katibu Mkuu 1, Makatibu Tawala wa Mikoa 3, Kamishna Jenerali wa Magereza na Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji.

Wengine ni Kamishna wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Msajili wa Mahakama Kuu na Wajumbe 3 wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Viongozi hao wataapishwa kuanzia saa 3:15 asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam na wanatakiwa kufikia Ikulu kabla saa 2:00 asubuhi kupitia lango la Mashariki (Lango la Baharini).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages