Wizara ya Ulinzi nchini Marekani (Pentagon) imetahadharisha juu ya ongezeko la kujiua maafisa wa jeshi la anga la nchi hiyo.
Katika indhari mpya ya Pentagon kuhusiana na ongezeko la kujiua askari wa nchi hiyo, viongozi wa jeshi la anga wametangaza kuwa kiwango cha kujiua ndani ya jeshi hilo kiliongezeka kwa asilimia 33 mwaka 2019 ikilinganishwa na mwaka 2018. Jeshi la anga la Marekani pia limeongeza kuwa jumla ya askari 137 wanaohudumu katika jeshi la anga na ambao ni walinzi wa taifa na akiba ya jeshi la anga walijiua mwaka jana. Brian Kelly, kaimu mkuu wa kitengo cha nguvu kazi, wafanyakazi na huduma za jeshi la anga nchini Marekani amesema kuwa, sio rahisi kufahamu njia za kukabiliana na ongezeko la kujiua kwa askari hao.
Hadi sasa Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetoa ripoti mbalimbali kuhusiana na ongezeko la vitendo vya kujiua askari wa nchi hiyo hasa katika miaka ya hivi karibuni. Viongozi wa kijeshi nchini humo wanayataja matatizo ya kisaikolojia kwa askari waliorejea kutoa maeneo ya vita kuwa chanzo kikuu cha kujiua askari hao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇