LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 9, 2020

NAIBU WAZIRI AWESO AZINDUA MRADI WA MAJI SAFI KATA YA MAKANG'WA

Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso,amewataka wananchi wa Kata ya Makang’wa kuutunza mradi wa maji wenye  thamani ya sh milioni 350 ambao unatoa lita 379,200 kwa siku zenye uwezo wa kuhudumia wakazi 7555 wa kata hiyo.

Na pia  amekabidhia sh milioni 100 kwa ajili ya kuongeza visima vingine viwili katika Kata hiyo ambavyo wataalamu wa Maji watafanya utafiti kujua wapi vichimbwe.

Wito huo ameutoa jana wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa maji safi katika kijiji cha Makang’wa uliogharamiwa na Wizara hiyo na kutekelezwa na Duwasa,amesena kuwa  kupitia Force Account inafanikisha kujenga miradi ya maji vijijini na mijini na kuokoa kero za maji kwa wananchi.

Mhe.Aweso ametoa pongezi kwa  Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira Duwasa kutokana na kutekeleza mradi huu kwa muda mfupi kwa gharama nafuu toafuti kama tungemkabidhi mkandarasi.

”Natoa pongezi zangu kwako  Mhandisi Pallangyo kwa sababu wewe na wataalamu wako mmefanya kazi kubwa mno kwa kuwapatia maji wakazi wa eneo hilo, “amesema Aweso.

Aidha Mhe.Aweso ameiagiza  kamati ya maji ya kata hiyo kuhakikisha inatoa ripoti ya mapato na matumizi ya fedha ambazo watauza maji kupitia mradi huo.

“Sitaki kusikia marumbano  ya mradi huu taarifa za mapato na matumizi ya mradi lazima zisomwe kwa wananchi ili waweze kujua, “amesisitiza Aweso.

Awali  Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi David Pallangyo amesema kabla ya kutekelezwa kwa mradi huu hali ya maji katika Kata hiyo haikuwa ya kuridhisha.

Mhandisi amesema kuwa  maji ya bomba yalikuwa yanapatikana katika kitongoji kimoja cha Sasi kati ya vitongoji 11 vya Makang’wa ambayo yalikuwa hayatoshelezi kabisa kwa wakazi wa eneo hilo na yaliwekwa na mtu binafsi.

“Wananchi wa karibu na eneo hilo walikuwa wanafuata maji kwenye kitongoji hicho kwa sh 200 kwa ndoo ya lita 20,lakini hivi sasa maji ya DUWASA ndoo mbili watalipia sh 50,”amesema Mhandisi Pallangyo.

Hivyo DUWASA imefanikiwa kumtua ndoo Mama kichwani kama kampeni yetu inavyosema.

   Kwa Upande wake  Mbunge wa Jimbo la Mtela Livingstone Lusinde amemshukuru Naibu Waziri kwa kuwapatia maji wakazi wa eneo hilo na kuondoa kero ya maji toka miaka 50 iliopita.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages