LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 9, 2020

MWAMPOSA ATANGAZA KUSITISHA MAKONGAMANO YA IBADA KUFUATIA VIFO VYA WAUMINI MKOANI KILIMANJARO

KAWE, Dar es Salaam
Kiongozi wa Kanisa la Inuka Uangaze, Boniface Mwamposa (Pichani), ametangaza kusitisha makongamano ya kiibada kufuatia  vifo  vya watu 20 na majeruhi 16 vilivyotokea Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro siku ya Jumamosi, Februari mosi mwaka huu baada ya kukanyagwa wakigombea kukanyaga mafuta ya upako yaliyowekwa katika milango ya kutokea  katika viwanja vya Majengo Mjini humo.

Mwanposa  ametoa tangazo hilo kabla ya kuanza kwa ibada katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, nakuelezea tukio lile la vifo vya watu 20 na 16 kujeruhiwa kuwa ni jaribu na ametoa pole kwa wale wote waliopoteza wapendwa wao na waliopatwa na majeraha na kueleza kuwa jambo hilo lilitokea akiwa ameshatoka Moshi  akiwahi Dar es Salaam kwa ajili ya Kongamono lingine.

“Kwa sasa makongamano mengi nimeyasimamisha kwa sababu ya jambo hili ambalo limetokea na tunaomba neema ya Mungu ikapate kusimama na watu na baada ya hapo ndipo nitaweka ratiba ya makongamano.” amesema Mwamposa.

“Leo Jumapili ilipaswa liwe kongamano kubwa la kukanyaga mafuta lakini kwa sababu ya shida iliyotokea, tumesimamisha yote kupata utulivu wa kuomba Mungu atupe neema ya kupanga mipango upya, nitaongea mengi kwenye ibada,” amesema Mwamposa na kuongeza;

Linapotokea jambo kama hili kila mmoja atazungumza lake, na hatuwezi kuongea mengi kwa sababu vyombo vya ulinzi na usalama vinachunguza jambo hilo, kwa hiyo nikiongea sana nitavuruga na kuharibu uchunguzi unaoendelea". 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages