LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2020

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TANZANIA BARA AZINDUA OFISI YA CCM MKOA WA GEITA

Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Ohilip Mangula akiteta jambo na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanalu Mstaafu Ngemela Lubinga wakati wa uzinduzi wa  jengo la  ofisi ya CCM mkoa wa Geita



15.02.2020
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Ndugu Philip Japhet Mangula amezindua jengo la ofisi ya CCM Mkoani Geita ambalo ni limejengwa na  viongozi wa Chama na Serikali, Wanachama wa CCM pamoja na wadau mbalimbali Mkoani hapo.

Aidha, Ndugu Mangula akiwahutubia wana CCM hao aliwaambia, kuelekea uchaguzi Mkuu wazingatie Amani, Upendo, Umoja na Mshikamano na kwamba Wabunge waliopo madarakani waachwe wamalize muda wao bila kuwasumbua mpaka Bunge litakapoahirishwa.

Ndugu Mangula pia aliwakabidhi vyeti vya shukurani kwa kutambua na kuthamini mchango wao wa hali na mali wale wote walioshiri na kuchangia kufanikisha ujenzi wa jengo hilo.

Naye, Katibu wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa) na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye pia ni Mlezi wa Mkoa wa Geita Ndg Ngemela Lubinga ametoa shukurani za dhati kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa uwakilishi wake alioutuma wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara katika uzinduzi huo.

Imeandaliwa na;
IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages