Mhe.Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna akizungumza katika maadhimisho ya kilele cha siku ya sharia Nchini katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Arusha mjini
Gwaride
maalum lililoandaliwa na Jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia
(FFU) Kwaajili ya maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini katika
viwanja vya Mahakama ya mwanzo Arusha Mjini
Naibu
Msajili Mfawidhi wa Mahakama kuu Arusha Sekela Mwaiseje akizungumza
katika siku ya Maaadhimisho ya siku ya sheria Mahakama ya Mwanzo Arusha
Mjini
SP Mikidadi Galilima - Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha akitoa salamu kwa Mhe.Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna kushoto kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana
Mhe.Jaji Mfawidhi
wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna kushoto kwake ji mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakiwa katika Maadhimisho ya siku ya
sheria nchini katika Mahakama ya Mwanzo Arusha Mjini.
Baadhi
ya Mhakimu wakiwa katika siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya
sheria nchini yaliyofanyika katika Mahakama ya mwanzo Arusha Mjini leo
Na Vero Ignatus, Arusha
Maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini
yamefanyika leo katika viwanja vya Mahakama ya mwanzo Mjini Arusha ambapo
madhumuni yake ni kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama,sambamba na
kuelimisha jamii kwa kuzingatia mada na iliyotolewa kwa mwaka husika
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna alisema kuwa kazi kuu ya na wajibu wa msingi wa Mahakama ni kutoaji haki kwa watu wote ambapo suala hilo siyo mambo ya Kisheria peke yake bali ni suala la Kikatiba.
Mhe.Mzuna alisema
Mahakama inatazamiwa kuharakisha usikilizaji wa migogoro inayohusiana na
wawekezaji na ya kibiashara ili hatima yake ifahamike mapema iwezekananyo na
hivyo kuruhusu shughuli nyingine za kimaendeleo na ukuaji wa uchumi kuendana
sawa na dira ya serikali.
“Hivyo basi serikali imejitahidi
kurekebisha mfumo wa uchumi kulingana na mazingira ya uchumi wa soko na
utandawazi ikiwemo kuweka mazingira ya kuwavutia wawekezaji mbalimbali vilevile
mahakama inatakiwa iende sambamba na mabadiliko hayo ambayo yanagusa eneo
muhimu la utoaji haki”
Aidha alisisitiza kuwa Mahakama imeweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa mashauri
hayachukui muda mrefu wala kuahairishwa pasipokuwa na sababu za msingi ambapo
katika Mahakama za mwanzo mashauri hayapaswi kukaa zaidi ya miezi sita, wakati
katika Mahakama za Hakimu Mkazi wa
wilaya mashauri hupaswa kuchukua muda wa miezi kumi na mbili kukamilika na kwa
upande wa Mahakama Kuu shauri halitakiwi kukaa si zaidi ya miaka miwili.
''Kuthibitisha hili kwa mahakama Kuu
Arusha mwaka juzi (2018)Mashauri yaliyomalizika yalitumia wastani wa siku 347
kwa mwaka 2019 ni wastani wa siku 397kwa muda wa miaka hiyo miwili wastani wake
ni siku 374 sawa na mwaka mmoja na mwezi mmoja (1.022185)’’Alisema
Nae Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Arusha Abdallah Chavula mfumo huru na madhubuti wa haki jinai
katika ukuaji wa uchumi ni kuongeza usalama wawananchi na kupunguza uhalifu
sambamba na kupunguza gharama za kiuchumi kwa serikali kutotumia uhalifu na
kupunguza gharama kwa serikali kutotumia fedha na rasilimali katika kulinda
jamii na mali zao dhidi ya vitendo vya kihalifu
Chavula alisema kuwa matunda ya
mfumo huo ni uwepo wa amani na utulivu katika jamii hivyo shughuli za uwekezaji
na biashara kuweza kufanyika kwa wepesi na mchango wawaendesha mashtaka katika
kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara ili
kusimamia na kuratibu kwa weledi shughuli za upelelezi,kuakikisha mashtaka
yanayofunguliwa mahakamani ni yale ya yenye ushahidi madhubuti na kuendesha
mashauri ya jinai bila ubaguzi wala upendeleo
Nae Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama kuu Arusha Sekela Mwaiseje alisema kuwa katika
wiki ya Sheria Mahakama na wadau wametoa elimu ya sheria sehemu mbalimbali
ikiwemo Mrisho Gambo sekondari,Muungano ,Ilboru,Chuo cha kilimo na mifugo
Tengeru Chuo cha Ufundi Arusha pia elimu hiyo imetolewa katika vyombo
mbalimbali vya habari mkoani hapa
Elimu hiyo iliyotolewa na mahakama imewafikia wastani wa wananchi 2565 ambapo
hesabu hiyo haijajumuisha wananchi mbalimbali ambao walisikiliza kupittia
vyombo vya habari
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇