LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 15, 2020

MADAKTARI NA MANESI 1700 NCHINI CHINA WAATHIRIKA NA VIRUSI CORONA

Taaifa iliyotolewa na kamisheni hiyo jana Ijumaa mjini Beijing imebaini kuwa zaidi ya watu 1,500 kati ya madaktari na manesi hao, wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Hubei ambapo 1,102 miongoni mwao waliambukizwa virusi hivyo katika mji wa Wuhan, makao makuu ya mkoa huo. Taarifa hiyo hiyo imeongeza kuwa idadi ya maafisa hao wa afya walioambukizwa virusi hivyo inalingana na asilimia 308 ya waathirika wote wa maradhi hayo. 

Madaktari wanaokabiliana na virusi vya Corona

Kamisheni ya Afya ya Kitaifa nchini China imeendelea kufafanua kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha kwa maradhi hayo hadi kufikia Ijumaa ya jana ilikuwa ni 1468. Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi akizungumza na vyombo vya habari kando ya mkutano wa usalama mjini Berlin, Ujerumani amesema kuwa uchumi wa China utafufuka kwa nguvu kubwa na kwamba virusi vya Corona vitasambaratishwa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages