LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 8, 2020

YAVURUMISHA MAKOMBORA YA BALESTIKI NA KUPIGA KAMBI ZA JESHI ZA MAREKANI

Jan 08, 2020 03:48 UTC
  • Iran yavurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za jeshi za MarekaniJeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limevurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.
Taarifa ya IRGC imesema kuwa, Iran imetoa jibu hilo kwa chokochoko za Marekani alfajiri ya leo, ambapo imelenga uwanja wa ndege wa kijeshi wa Marekani wa Ain al-Assad katika mkoa wa al-Anbar, magharibi mwa Iraq.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limeitaka Marekani iwaondoea wanajeshi wake wote katika nchi hiyo ya Kiarabu, likisisitiza kuwa halitatenganisha kati ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kujibu mapigo ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Soleimani.
IRGC imeonya kuwa, "Shetani mkubwa, yaani utawala wa kiistikbari wa Marekani utakabiliwa na vipigo vikali vya kuumiza, iwapo utachukua hatua nyingine ya kichokozi dhidi ya taifa kubwa la Iran. Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imeongeza kuwa, pigo hilo dhidi ya Wamarekani wavamizi ni ushindi mkubwa kwa umma wa Kiislamu n taifa kubwa lisolotetereka la Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif ameashiria jibu hilo la Iran katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuandika: "Iran imechukua hatua madhubuti ya kujihami kwa mujibu wa Sura ya 51 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa kulenga kambi ya jeshi ambayo ilitumiwa katika shambulizi la kioga dhidi ya raia na maafisa wetu wa ngazi za juu. Hatutaki kushadidisha mambo wala vita, lakini tutajihami dhidi ya uvamizi wowote."
Kambi ya jeshi la Marekani iliyopigwa na akombora ya Iran mkoani al-Anbar
Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imethibitisha habari hizo za kuvurumishwa makumi ya makombora ya balestiki kuelekea katika kambi ya kistratajia ya jeshi la Marekani nchini Iraq.
Mapema jana, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema kisasi cha taifa la Iran kwa damu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha kitakuwa kikali, madhubuti, cha kutisha na kamilifu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages