LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 6, 2020

WAKAZI WA ILEMELA MKOANI MWANZA WAPATA KIVUKO KIPYA

 Kivuko kipya cha MV. Ilemela kikielea majini mara baada ya kushushwa , kivuko hicho ambacho ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.7 za Kitanzania kitakua kikitoa huduma kati ya Kayenze na Kisiwa cha Bezi na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano) Mhe. Atashasta Nditiye katikati akiwa ameshikana mkono na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza zoezi za kushusha kivuko kipya cha Kayenze na 
kisiwa cha Bezi kilichogharimu shilingi bilioni 2.7 ambacho kimepewa jina MV.Ilemela, 
tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro Ilemela jijini Mwanza. Kushoto kwa Mongella ni Mbunge wa Iilemela Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Mhe. Angelina Mabula na wa tatu kushoto ni Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Japhet Maselle. Kivuko cha MV.Ilemela kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.
 Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano) Mhe.  Atashasta Nditiye katikati akifurahia jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle wa pili kushoto mara baada ya kumaliza zoezi la kukagua na kukishusha kwenye maji kivuko cha MV.Ilemela. Kivuko cha MV.Ilemela kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100 na kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni2.7.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akisoma taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa kivuko cha MV.Ilemela wakati wa hafla ya kukishusha majini kivuko hicho iliyofanyika katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella na katikati ni Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na awasiliano 
(Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano) Mhe.  Atashasta Nditiye. Kivuko cha MV.Ilemela kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100 na kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni2.7.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages