LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 13, 2020

UCHAGUZI WA BUNGE ETHIOPIA KUFANYIKA MEI AU JUNI MWAKA HUU

Hakikisho hilo limetolewa na Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia katika mkutano wake na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na kusisitiza kuwa, ratiba kamili ya uchaguzi huo itatolewa na Tume ya Uchaguzi.
Uchaguzi huo wa Bunge unatarajiwa kuwa wa kwanza chini ya uongozi wa mshindi huyo wa tuzo ya Nobel ambaye alichukua wadhifa wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Aprili mwaka 2018.
Waziri Mkuu wa Ethiopia ameeleza kuwa nchi yake inakabiliwa na changamoto nyingi siyo vifaa vya uchaguzi tu, bali kuna changamoto nyingine kama za usalama na amani.
Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini
Aidha amewataka wananchi wa Ethiopia pamoja na vyama vya siasa vya nchi hiyo kusaidia ili uchaguzi huo ufanyike katika mazingira ya amani na demokrasia.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, vyama vya upinzani nchini Ethiopia vimetahadharisha kuhusiana na hatua yoyote ile inayolenga kuakhirisha uchaguzi huo wa Bunge.
Tangu alipochukua uongozi nchini Ethiopia, Abiy Ahmed amefanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kisiasa na kumletea sifa kubwa kieneo na kimataifa, ingawa mabadiliko hayo yamepelekea pia kuibuka machafuko katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages