Jan 3, 2020

TAARIFA YA AJALI YA GARI KUUNGUA MOTO NA KUSABABISHA MAJERUHI NA UHARIBIFU WA MALI MKOANI MBEYA.



Mnamo tarehe 02.01.2020 majira ya saa 16:05 jioni huko eneo la Meta-Igurusi katika barabara kuu ya Mbeya/Njombe,   Gari lenye namba za usajili T. 956 DRT/T. 886 DRV aina ya Scania Tanker la Mafuta mali ya kampuni ya â€śworld oil” lililokuwa limepakia mafuta aina ya Petroli kutokea Dar es salaam kuelekea nchini Zambia likiendeshwa na dereva ISSA YUSUPH [35] mkazi wa Jijini Dar es Salaam lilipata hitilafu za kiufundi siku ya tarehe 01/01/2020 majira ya saa 16:30 jioni na baadae liliungua moto na kuteketea wakati wa harakati za kufaulisha mafuta kwenye gari hiyo kwenda kwenye gari namba T 844 AWJ Trailer na kusababisha majeraha kwa watu wawili.

Watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo ya moto ni:-

1.    JULIUS DAUDI [30]
2.    STANFORD MWAKYUSA [45] 

wote wakazi wa Igurusi Wilayani mbarali.
Aidha katika ajali hiyo kulitokea uharibifu kwa gari namba SM 4633 aina ya Isuzu mali ya Jeshi la Zimamota na Uokoaji na gari namba T 844 AWJ Trailer. Chanzo cha ajali ni mlipuko uliotokea kwenye mashine ya kufaulishia mafuta aina ya “water pump”. Majeruhi wamekimbizwa kituo cha afya igurusi kwa matibabu.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.




No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages