LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 12, 2020

SHANGWE LA SHULE ILIYOONGOZA KITAIFA MATOKEO KIDATO CHA NNE LAFUNGA MITAA BUKOBA



Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV

Kufuatia matokeo ya Mitihani ya Kitaifa yaliyotangazwa Mwishoni mwa Wiki hii na Baraza la Mitihani la Taifa, yakibainisha Ushindi mnono wa kishindo kwa Shule za Sekondari na Msingi za Kaizirege na Kemebo's, Wafanyakazi pamoja na Wanafunzi wa Shule hizo wameitumia Jumamosi ya Januari 11, kufunga Mitaa ya Bukoba Manispaa kwa maandamano na kidedea cha Ushindi kufurahia Matokeo hayo.

Msafara huo ukiongozwa na Gari la Polisi umeonekana ukikatiza maeneo mbalimbali ya viunga vya Manispaa ya Bukoba, katika kusherekea Ushindi huo wa matokeo ya Darasa la Nne, Kidato cha Pili na Kidato cha Nne, ambapo Shule hizo zimefanya Vizuri kwa Kushika nafasi ya Kwanza Kitaifa mtihani wa Darasa la Nne, nafasi ya Pili Kitaifa Mitihani wa Kidato cha Pili, na nafasi ya Kwanza Kitaifa Mitihani wa Kidato Cha Nne.

Akizungumza kwa nyakati tofauti Meneja wa Shule hizo Bwn. Rodgers M. Katiti amesema mbali na jitihada zilizofanywa na wanafunzi pamoja na walimu, siri kubwa ya Ushindi wao ni kujituma, lakini Uongozi kuwa karibu na wafanyakazi kwa kuwapa stahiki zao kwa wakati, kupanga mikakati madhubuti na kujipangia majukumu, na kuwa kushika nafasi hizo Kitaifa sio kazi kubwa, kazi ni namna ya kuendelea kuitunza nafasi isikuponyoke, na hivyo tayari mikakati imeanza kwa matokeo yajayo.
 Pichani ni Ndinga ya Mama Mkurugenzi wa Shule za Kemebo's ikiwa na Bango Nyuma linalosomeka "TANZANIA ONE" hii ni kumaanisha Ushindi wa Kwanza Kitaifa kama lilivyokonekana kukatiza mitaani.
 Pichani ni Vibe la wanafunzi wa Kemebo's wakisherekea Ushindi wa matokeo yao ya Kidato cha Pili ambapo wamekuwa wa Pili Kitaifa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages