Na Khadija seif, Michuzi Tv
TIMU ya Namungo fc waahidi kuonyesha maajabu kesho katika mchezo wao dhidi ya wekundu wa msimbazi Simba fc.
Akizungumza hayo mara baada ya kutia saini
makubaliano ya udhamini wa Kampuni ya ubashiri ya sportpesa baina ya
timu ya Namungo Mwenyekiti wa timu hiyo Hassan Zidadu amewashukuru
sportpesa kwa udhamini huo na kuhaidi kufanya vizuri kutimiza malengo ya
udhamini huo.
"Kupewa kwetu udhamini huu ni furaha na itakua chachu kwetu kufanya
vizuri zaidi na kuhakikisha timu ya namungo inafika mbali zaidi ili
Kampuni ya sportpesa wahamasike na kushawishika kuongeza donge nono
zaidi ya hili".
Hata hivyo Zidadu ameeleza kuwa kuelekea mchezo wao dhidi ya klabu ya
simba na kuwahakikishia wapenzi wa namungo kuwa wamejipanga vizuri
kuwakabili Simba.
"Kesho maajabu sio Simba kuifunga namungo
bali maajabu yatakua namungo kuifunga Simba hivyo mashabiki wajitokeze
kwa wingi kushuhudia mtanange huo ".
Pia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya ubashiri ya
sportpesa nchini Abbas Tarimba akiweka bayana udhamini huo uliogharimu
shilingi za Kitanzania milioni 120.
"Tumeamua kudhamini timu ya namungo kutokana na weledi wake pamoja na
bidii na wapo nafasi nzuri kwa sasa kwenye ligi kuu ambapo wapo nafasi
ya tano na tumetoa udhamini wa milioni 120 na sio Mwisho tu tukiona
wanafanya vizuri tutegemee dau litapanda zaidi,"
Mwenyekiti wa timu ya Namungo akitoa neno la shukrani kwa Kampuni
ya ubashiri sportpesa jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini mkataba
wa udhamini kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya
ubashiri sportpesa na kushoto ni katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa
miguu (TFF) Wilfred kidao jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇