Na Maiko Luoga Mbeya
Naibu
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson
Januari 21, 2020 alifanya ziara ya Kikazi katika kituo kikuu cha Mabasi
mkoani Mbeya kwa lengo kutimiza ahadi yake ya kuwapatia Sare maalumu za
kuwatambulisha maafisa usafirishaji katika jiji la Mbeya.
Maafisa
hao maarufu kama Wapigadebe, wamepewa Sare hizo ili kuwaepusha na kero
za kukamatwa mara kwa mara na Askari wa Jiji la Mbeya wakiwa hawana
utambulisho maalumu wa kazi wanazozifanya wawapo kwenye Majukumu yao.
Aidha
Dkt. Tulia amejionea na kuelezwa Changamoto mbalimbali zilizopo katika
kituo hicho kikuu cha Mabasi ikiwemo ukosefu wa maji, ubovu wa
miundombinu ya vyoo, uhaba wa taa kwaajili ya mwanga Majira ya usiku
pamoja na Runinga maalumu ya kuwawezesha kufuatilia Taarifa na Matukio
mbalimbali ya Kitaifa.
Changamoto
nyingine ni pamoja na Ukosefu wa Vitendea kazi vya kubebea Mizigo ndani
ya Stendi ikiwemo Toroli huku wakimuomba Naibu Spika Dkt, Tulia Ackson
kuwawezesha upatikanaji wa mikopo kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust.
Baada
ya kuzungumza nao Dkt. Tulia ameahidi kushirikiana na Maafisa hao
katika kutatua changamoto hizo huku akiwakabidhi Toroli moja la kubebea
mizigo, kununua Taa za kufunga maeneo yanayozunguka kituo hicho cha
Mabasi na kueleza kuwa atafanya jitihada za kuhakikisha huduma ya maji
inapatikana kwa haraka Kituoni hapo.
“Ndugu
zangu niseme tu kwamba nimezisikiliza changamoto zenu na sisi kama
Tulia Trust tunaahidi kushirikiana na Serikali yetu inayoongozwa na Rais
Dkt, John Pombe Magufuli kuhakikisha tunawakomboa vijana katika janga
la umasikini, na hata hili suala la mikopo vijana wa Tulia Trust
watakuja hapa na kuwapa huduma”-Alisema Dkt, Tulia Ackson Naibu Spika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇