LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 8, 2020

MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Watumishi wa Umma nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kufanikisha juhudi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli za kukuza uchumi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida katika ziara ya kikazi mkoani Singida.


Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa ni lazima watumishi wa umma waheshimu kazi na wahakikishe wanatimiza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo kwa kuwa Serikali ya Awamu ya tano haitovumilia watumishi wazembe.

“Mtumishi wa Umma ni tunu kwa hiyo ni bora ukachezea mshahara kuliko kuchezea kazi kwa sababu wapo wanaotamani kuingia serikalini lakini hawana fursa hiyo” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Dkt. Mwanjelwa ametoa wito kwa Watumishi wa Umma nchini kufanya kazi kwa kuendana na spidi ya Mheshimishimi Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na si kwa kulegalega.

Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni ya uadilifu, utendaji kazi uliotukuka , haki na haiko tayari kumuonea mtumishi yeyote.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka Watumishi wa Umma kuwa na subira katika kipindi ambacho serikali inafanyia kazi changamoto zao za  malimbikizo ya mishahara, kupandishwa madaraja na nyinginezo.

Mhe.Dkt. Mwanjelwa yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Singida kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAF na kukutana na Watumishi kwa lengo la kusikiliza maoni na kutatua kero zao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages