NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
MWANAMKE mmoja huko jiji la Vatican ameung’ang’ania mkono wa Papa Francis alipokuwa akiwasalimia watoto na waumini baada ya kuongoza ibada ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2020 kwenye kanisa la St. Peter.
Naye Papa akiwa na hasira kutokana na kitendo hicho, ili kujinasua alilazimika kuuchapa kofi mkono wa mwana mama huyo.
Mwana mama huyo hatimaye aliauachia mkono wa Papa.
Baada ya tukio hilo, Papa Francis aliomba radhi kwa kutokwa na subra na kufanya kitendo hicho cha kuuchapa kofi mkono wa mwanamke huyo.
“Upendo hutufanya kuwa na subira, kwa hivyo mara nyingi tunatokwa na subira hata mimi na ninaomba radhi kutokana na kitendo kibaya cha jana (Jumatano).” Alisema Papa Francis
Akieleza zaidi Papa alisema wanawake ni chanzo cha maisha, lakini bado wananyanyaswa, wanapigwa, wanabakwa na wanalazimishwa kufanya ukahaba na hivyo kuukandamiza uhai walioubeba kwenye matumbo yao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇