Na Mwandishi Wetu,Michuzi Globu ya jamii
KABLA ya Rais Dk.John Magufuli hajatangaza kumuondoa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola leo Januari 23 mwaka huu 2020, Waziri huyo akipata bahati ya kutoa salamu zake za mwisho akiwa kwenye nafasi hiyo.
Wakati shughuli za uzinduzi wa nyumba za askari magereza ukiendelea na kabla ya Rais kuzungumza na Watanzania, viongozi mbalimbali walipata nafasi ya kutoa salamu kwa Rais na miongoni mwao alikuwepo Kangi Lugola ambaye alitumia nafasi hiyo kueleza mengi huku akimiminia sifa Dk.Magufuli kutokana na utendaji wake wa kazi.
Huku
akiwa amevalia suti yake Nyeusi ya mikono mifupi akiwa ameshikilia
Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akitumia muda wa dakika nane
kuzungumza.
Kwa kukumbusha tu maneno ya Kangi Lugola ambayo ni ya mwisho kuyatoa kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ni haya hapo chinNa Mwndishi.
Kwa kukumbusha tu maneno ya Kangi Lugola ambayo ni ya mwisho kuyatoa kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ni haya hapo chinNa Mwndishi.
Alianza kwa kusema Tanzania hoyeeeeee............
Magufuli hoyeeeee.......
Nani kama Magufuliiiii...... nani kama Magufuliiii....... ( huku akipunga mkono)
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Mama yetu mama Janeth Magufuli, Mke
wa Rais, Mheshimiwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Mkuu wa
Majeshi ndugu yetu Mabeyo, lakini kwa umhimu kabisa Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda, ambaye ametupa salamu za timu ya Yanga kule
Singida, lakini niseme tuu kwamba hata kule Singida walibaki na amani
walioidumisha kutokana na kukubali matokeo ya kufungwa na Yanga.
Kwahiyo amani watanzania tumefika mahala pale tunapofungwa wanatunza amani, Itifaki imezingatiwa.
Mheshimiwa
Rais nianze na Jambo moja kwabisa la kuwakumbusha watanzania, juu ya
kitabu hiki ambacho ni maarufu kwa jina la Ilani ya Chama cha Mapinduzi
(CCM),(Huku akipunga Kitabu cha Ilani ya CCM) kwaajili ya Uchaguzi wa
2015.
Mheshimiwa Rais kitabu hiki ni Mkataba baina ya chama cha Mapinduzi ibala ya pili pamoja na wananchi wapiga kura wa Tanzania.
Lakini
Mheshimiwa Rais Kitabu hiki Ibala ya Nne wakati unazunguka nchi nzima,
uliwaahidi watanzania kwa mujibu wa wa Ibala ya Nne.
Kwamba
Serikali yako ya awamu ya tano itahakikisha kuna amani, itahakikisha
kuna usalama, na utulivu wa hali ya juu na uliwahakikishia kwamba maisha
ya wananchi pamoja na mali zao vitalindwa kwa nguvu zote za serikali.
Mheshimiwa
Rais, naomba kwa unyenyekevu niuthibitishie Umma wa watanzania,mija
wapo ya wizara ulizoziunda, katika kutekeleza jambo hili la amani,
usalama na utulivu na maisha ya watu na mali zao ni wizara ya mambo ya
ndani ya nchi.
Mheshimiwa
Rais tukiwa tunawaambia watanzania, tukiwa tunawathibitishia
watanzania, kwamba pamoja na n kwamba bado tunamuda mfupi wa kumaliza
miaka mitano lakini Dkt. John Pombe Magufuli, ameweza kutekeleza ilani
hii kuhakikisa nchi hii imetulia mahala pake.
Mheshimiwa
Rais kulikuwa na matukio ya ujambazi wa kutumia siraha na bundukil leo
mheshimiwa Rais imekuwa ni historia wananchi wanalala bila kusikia milio
ya bunduki tumpigie makofi matatu Mheshimiwa Rais(Mhuku akiwa
amenyanyua mikono juu kuashiria kupiga makofi).
Mheshimiwa
Rais kulikuwa na ajali nyingi sana za barabarani lakini Mheshimiwa Rais
uliendelea kutuhimiza wizara yako, na sisi tukasema hatutakuangusha, na
ndio maana leo Mheshimiwa Rais ajali ambazo zinachukua maisha ya watu
wengi pamoja na mali zao, sasa zinaenda ukingoni.
Na
ndio maana Mheshimiwa Rais zamani tulifika pahala wananchi tukawa
tunaogopa majambazi, kusafiri Nyakati za usiku, tulikuwa tunaogopa
majambazi hata baadhi ya maeneo kwenda, tukafika pahala kana kwamba
kwamba majambazi ndio yanapanga ratiba za watanzania, ni saa ngapi
watakuwa watanzania watakuwa wanafanya kazi, tulifika pahala majambazi
yakatupangia ratiba ya mabasi yasafiri saa ngapi na maeneo gani.
Mheshimiwa
Rais nataka niuthibitishie Kwa niaba ya Serikali yako umma wa
watanzania, leo mwananchi anauesafiri kutoka mikoa ya kaskazini anaenda
Mbeya anaens Songea anasafiri anatoka Mikoa ya Dar ea salaam anakwenda
kanda ya ziwa, Mwnza wanatoka Arusha leo wanasafiri bila wasiwasi masaa
24 makofi matatu kwa mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Mheshimiwa
Rais kumekuwa na maneno ya watu wanasema fedha ambazo unawaambia
unakusanyabza kutosha kwaajili ya nchi hii na kwamba nchi hii umeipaisha
sasa katika uchumi wapo watu ambao pengine pamoja na kwamba wanaona
lakini hawataki kukubali matokeo nataka niwahakikishie kwamba ibara ya
146 (Huku akiwa wameishika juu Ilani ya Chama cha CCM) katika Ilani
hii mambano ndogo tano uliwahakikishia watanzania kwamba vyombo vya
ulinzi na usalama, utavipatia makazi kwaajili yabkujenga ari na morali
kwa askari kwaajili ya kuendelea kulinda nchi hii amani na usalama wa
nchi hii.
Mheshimiwa
Rais, nawathibitishia umma wa watanzania kwamba kama kuna wakati
mheshimiwa Rais, umevisaidia vyombo vya ulinzi na Usalama kwenye eneo la
makazi ni katika kipindi hiki, katika serikali yako ya awamu ya tano na
ndio maana vyombo vya ulinzi na usalama iwe ni Polisi, kila kukicha
majengo ambayo yanatupa fedha tunaendelea kuyazindua, tunakuwa na
majengo ya uhamiaji, tunakuwa na majengo ya zima moto na leo Mheshimiwa
Rais jeshi la magereza Tanzania, katika historia ambayo leo unaenda
kuiandika, walikuwa na majengo duni, tangu mkoloni alipo acha jeahi la
magereza hapa, hawakuwahi kuwa hata nyumba moja ya ghorofa, leo
Mheshimiwa Rais umetujengea maghorofa ambayonumeandika historia, ambapo
vijana wetu sasa wataenda kuishi na kufanya kazi kwa moyonmkubwa na ari
kubwa.
Na
nimalizie kwa kusema Mheshimiwa Rais ilipotupatia fedha bilioni 10
kijenga makazi haya ya Askari yalikuwa yamelenga kujengamaghorofa manne
katika nyumba moja ya brock moja lakini TBA walipokija hapa hatukuweza
kutimiza azima hiyo, lakini naamini alipita hapa ibirisi shetani na
jeshi lake, na ibirisi shetani alipokuja akakalia site, ndio maana TBA
walikuwa na kigugumizi, kwa sababu walikuwa wamepigwa upofu, lakini
Mheshimiwa Rais, wewe kama Amili Jeshi Mkuu ulipo tinga hapa ukiwa na
majeshi mawili jeshi la Mungu pamoja na Jeshi lako lako ulinzi wa
wananchinwa Tanzania na JKT, jeshi la ibilisi shetaniwaliweza kukimbia
na kuiacha site, na ndio maana site hii ilikaliwa na majeahi yako na
matokeo yake Mheshimiwa Rais tumeyaona ambapo leobunaenda kutukabidhi
nyumba hizi na wale wanaoendelea kubeza juhudi zako Mheshimiwa Rais,
wale ambaowanaona kwambabmacho yao hayaoni, lakini tunawaambieni, siku
za serikali awamu ya tano zinafikia mwisho.
Watanzania
wenye imani, watanania wenye moyo watanzania wanaokuunga mkono ni
asilimia 99.1 ako 0.1ni wale ambao mioyo yao imeshikiliwa na adui
shetani lakini na wao pia kwa jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye
hai washindwe na walegee, na ninawafungua kwa minyororo ya upofu ili na
hiyo asilimia waweze kukubali kazi unayoifanya.
Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli namalizia kwa kusema kwa kuwa katika kipindi
hiki watanzania wamekuweka juu ukang'araaa.... Ahaaa imekula kwao
utaendelea kuwa juuuu tena juuu zaidi. Magufuli hoyeeeee.
Mheshimiwa
Rais nakushukuru kaa nyumba hizi kama nilivyotangulia kusema, hatuna
sababu ya kuendelea kuwa omba omba wa nyumba hizi kwa sababu Mheshimiwa
Rais unasimamia miradi yetu, unaifahamu na uchungu nayo na ndio maana
unaendelea kumwaga fedha na hizi fedha unazozimwaga kwenye vyombo vya
ulinzi na usalama, zile huduma wanazozitoa na matokeo ya amani na
utulivu unaoona ndizo fedha za walipakodi zinazowafikia wananchi kwa
njia ya huduma.
Na
ninataka niwaambie watanzania, siku mkibeza juhudi hizi zinazofanywa
na kupitia amani ikakatika, usalama ukakatika fedha zote Mheshimiwa
Rais atazielekeza kununua malisasi, kununua mabomu kwaajili ya kulinda
nchi, matokeo yake hatutajenga hospitali, watu hawatajenga shule, watu
hawatalima na matokeo yake nchi itakuwa masikini.
Magufuli hoyeeee...... Asanteni sana.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇