Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NYOTA
wa timu ya vijana ya Azam FC 'Azam U-20' na timu ya Taifa ya Vijana
'Ngorongoro Heroes', Tepsi Evance, amewasili nchini Ufaransa kwa ajili
ya kujiunga na timu ya Nantes.
Tepsi
aliondoka jana pamoja na wakala anayetambulika na Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA), Kambi Seif kwenda Nantes kwa ajili ya mafunzo hadi
atakapotimiza umri wa miaka 18 baadae mwaka huu asaini mkataba.
Evance
atakapofikisha umri huo, atajiunga moja kwa moja na timu ya wakubwa ya
Nantes inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo (Ligue 1).
Tepsi Evance akiwa makao makuu ya klabu ya Nantes baada ya kuwasili Ufaransa jana
Tepsi ni mmoja kati ya vijana wanne waliopatikana kwenye usahili uliofanywa na Cambiasso Sports na Rainbow Sports Novemba mwaka jana, kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mchezaji
mwingine wa Azam U-20, aliyefuzu kwenye usahili huo ni nahodha, Samuel
Onditi, ambaye anasubiria taratibu za Visa zikamilike sambamba na
wachezaji wengine wawili.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇