Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Angel Akilimali leo amekutana na Viongozi wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala na kuzungumza nao masuala mbalimbali ikiwemo kuimarisha Jumiya hiyo ya UWT na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa jumla.
Angel ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Taifa ya CCM na Mkuu wa Idara ya Siasa na Habari ya vyombo vya habari vya CCM vinavyosimamiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) alikutana na Viongozi hao wa UWT alipokwenda kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kujitambulisha rasmi kwa viongozi hao kufuatia kuhamishia makazi yake katika wilaya hiyo akitokea Wilaya ya Kigamboni.
Pichani, Angel akisaini kitabu cha wageni wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Katibu wa UWT Wilaya ya Ilala Bora Ngaraba. PICHA ZAIDI>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇