Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Rukwa imefungua Madawati ya watoto kwa baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari katika Manispaa ya Sekondari kwa lengo la kupambana na ukatili dhidi ya Watoto ikiwemo mimba za utotoni.
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea na wanafunzi wa shule za Msingi Chem chem na Lukewile zote Manispaa ya Sumbawanga ameutaja Mkoa wa Rukwa kuwa na changamoto kubwa ya mimba za utotoni.
Aidha Bw. Kitiku amewataka watoto shuleni hapo kulitumia Dawati la Watoto Shuleni hapo ipasavyo ili liweze kuwa masaada mkubwa kwa wanafunzi wanaokumbana na vitendo vya ukatili na kuwataka kutokuwa waoga wa kutoa taarifa ili kuwawezesha walimu wa malezi shuleni hapo kuweza kuangalia namna bora ya kulifanyia kazi taio hilo.
Bw. Kitiku ameongeza kuwa watoto wanatakiwa kupewa haki zote kama ilivyo kwa watu wazima akizitaja haki hizo kuwa haki ya kulindwa, haki ya kuendelezwa, Afya, kutobaguliwa na kushirikishwa kama ilivyobainishwa katika Sera ya Taifa ya Mtoto ya Mwaka 2008.
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka watoto hao kutoa taarifa katika Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi lakini pia kutumia mtandao wa simu ya bure ya 116 ili kuweza kupewa msaada wa haraka pindi watakapobaini kuwa wanafanyiwa vitendo vya ukatili ambavyo amevitaja kuwa ulawiti na ubakaji, kazi ngumu kwa watoto pamoja na utumikishwaji watoto manyumbani kwa maana ya ukatili wa kingono na kimwili.
Dwati la watoto katika shule hizo limefanyika kwa wanafunzi husika kuchagua wawakilishi wao ndani ya Dawati lakini pia wanafunzi hao baada ya kuelimishwa pia wamewachagua walimu ambao wanawaamini kuwa walezi hao ambao kimsingi watafanya kazi kwa karibu sana na Dawati la Jinisia shuleni hapo.
Zoezi la uanzishwaji Dawati la Watoto shuleni pia limefanyika shule ya Sekondari Kilimani Maweni iliyoko nje kidogo ya mji wa Sumbawanga na Wizara kwa kushirikiana na uongozi wa shule na mkoa wameongoza wanafunzi shuleni hapo kuchagua wawalilishi wao wa Dawati lakini pia wamechagua walimu wawili kuwa walimu wa malezi shuleni hapo.
Wataalam wa Wizara ya Afya Idara Kuu Mawendeleo ya Jamii wako Mkoani Rukwa kushirikiana na Mkoa huo katika juhudi zake za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na mkoa ni miongoni mwa mikoa yenye kiwango cha juu Kitaifa kuwa na idadi kubwa ya mimba za utotoni.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇