Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba
(TMDA), Adam Fimbo akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo
pichani), kuhusu mafanikio ya Mamlaka hiyo katika miaka minne ya
Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa
Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba nchini TMDA , imetambulika na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika
ubora wa udhibiti wa dawa na kuifanya Tanzania kupitia mamlaka hiyo kuwa ya kwanza barani Afrika
kufikia mafanikio hayo na imekuwa mshindi wa kwanza kwa ubunifu wa mfumo wa utoaji huduma kwa
wananchi katika wiki ya Utumishi wa umma barani Afrika mwaka 2019.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo,
alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia mafanikio ya Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka
minne.
Amesema katika kipindi hicho TMDA imefanikiwa kushikilia cheti cha kimataifa cha ithibati cha ISO
9001:2015 ambapo maabara ya Taasisi hiyo inatambuliwa na shirika la Afya Duniani kutokana na ubora
na umadhubuti wa kazi zake.
“Katika kipindi cha Miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, sisi
kama taasisi tumefanya mambo mengi makubwa ambayo yameleta mageuzi katika masuala ya udhibiti
na usalama wa Dawa na vifaa tiba, na tumeimarisha na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato”
Alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa TMDA.
Aidha amesema TMDA imesajili zaidi ya bidhaa 20,247 za dawa na vifaa tiba baada ya kujiridhisha ubora
,usalama na ufanisi wake hivyo kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa kwaajili ya kulinda afya za
watanzania.
Mamlaka pia imeimarisha udhibiti wa bidhaa kwa asilimia 96 katika kipindi cha mwaka 2015 hadi
Novemba 2019 hivyo kuifanya nchi yetu kuwa salama, pia mamlaka imeweza kusogeza huduma karibu
na wananchi kwa kujenga maabara ya kisasa Jijiji Mwanza.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa TMDA amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuwekeza
katika taasisi hiyo ili kulinda afya za watanzania , kwa kuongeza bajeti kutoa Shilingi Bilioni 34.64 mwaka
2015/16 hadi Shilingi Bilioni 53.31 kwa mwaka 2018/19 ambayo ni sawa na asilimia 53.8.
Mafanikio hayo yamewezesha kuimarika kwa huduma pamoja na kiuwezesha taasisi kutoa gawio kwa
serikali kila mwaka hadi kufikia shilingi Bilioni 29.1 katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu
ya Tano.
Katika kuelekea Tanzania ya Viwanda TMDA imetoa msaada wa kiufundi katika kuanzishwa kwa viwanda
vipya 12 vya dawa na vifaa tiba hivyo kuchangia katika juhudi za kukuza uchumi kupitia viwanda, na
katika kutimiza adhma hiyo imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki katika utoaji wa vibali ambapo
hutolewa kwa saa 24.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Afya iliyoundwa kwa
mujibu wa Sheria baada ya kufanyiwa marekebisho ya kiutendaji ya aliyokuwa Mamlaka ya na baadhi ya
majukumu yake kuhamishiwa katika shirika la Viwango Tanzania TBS.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇