Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Chato.
Katika ziara hiyo Waziri Ummy, ameongea na Wananchi waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali hiyo, huku akibaini changamoto ya uchache wa Watoa huduma za Afya katika Hospitali hiyo, licha ya jitihada za Serikali za kuongeza Watumishi wapya.
"Changamoto kubwa nilioiona ni Watumishi, nadhani wengi mmeshakaa zaidi ya masaa matatu tangu mmefika kupata huduma, sisi muongozo hausemi ukae zaidi ya masaa matatu, kwahiyo hilo tumeliona na tutaendelea kulifanyia kazi" alisema Waziri Ummy. Mbali na hayo, Waziri Ummy amewataka Wananchi waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali hiyo, kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya, na kuwaunga Watoto wao "Toto Afya kadi", ili kukabiliana na changamoto ya gharama kubwa za matibabu.
Aidha, Waziri Ummy amesema, Serikali inaendelea kuongeza Vituo vya kutolea huduma za Afya na kuboresha miundombinu chakavu ili kuhakikisha Wananchi wa hali zote wanapata huduma za Afya Bora na sahihi bila wasi wasi.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇