Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
George Simbachawene akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya
Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
George Simbachawene akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya
Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa TAREA, Mhandisi Prosper Magali.
Makamu Mwenyekiti wa TAREA, Mhandisi Prosper Magali(kulia)
akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya
Siku ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Jeroen Verheul akizungumza
kwenye uzinduzi wa Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu
yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
George Simbachawene akiangalia majiko yaliyotengenezwa kitaalamu kulinda
mazingira na yanatumia mkaa na kuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
George Simbachawene akitembelea mabanda mbalimbali kwenye Maonesho ya 14
ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu yanayofanyika Mnazi Mmoja,
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
George Simbachawene akiangalia jiko linalolinda mazingira kwenye moja ya
mabanda katika Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku ya Nishati Jadidifu
yanayofanyika Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),
George Simbachawene, ameiagiza Jumuiya ya Wadau wa Nishati Jadidifu
Tanzania (TAREA) kufanya utafiti katika Jiji la Dar es Salaam ili
kubaini kiasi cha matumizi ya nishati jadidifu.
Alitoa agizo hilo wakati akifungua Maonesho ya 14 ya Kitaifa ya Siku
ya Nishati Jadidifu yaliyofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam yakiwa na
kauli mbiu: “NISHATI JADIDIFU KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA 2025”
yaliyoandaliwa na TAREA na kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar
Salaam.
Aidha, ameyataka mataifa yaliyoendelea kuacha kuleta bidhaa chakavu
za kielektroniki zikiwamo runinga na friji katika nchi zinazoendelea
ikiwamo Tanzania kuacha kwa kuwa ni majanga.
Alikuwa
akijibu risala ya TAREA iliyosomwa kwake na Makamu Mwenyekiti wa TAREA,
Mhandisi Prosper Magali aliyesema licha ya TAREA na wadau mbalimbali
kuhamisisha matumizi teknolojia ya nishati jadidifu, zipo changamoto
kubwa za kudhibiti taka zitokanazo na bidhaa za kielektroniki zikiwamo
runinga na friji.
Simbachawene alisema inasikitisha kuona vifaa vilivyotumika na
kuchakaa katika mataifa yaliyoendelea bado zikiwamo friji na TV bado
zinaletwa katika mataifa yaliyoendelea ikiwamo Tanzania.
Akasema: “Kwa nchi zilizoendelea, kama kitu ni kibaya, tusikitumie
wote; tusione ni kibaya tukapeleka Afrika maana madhara yake tabaka la
ozini ni makubwa. Uchafuzi wa hali ya hewa husababisha kumomonyoka kwa
tabaka la ozoni na kubadilika kwa tabianchi huathiri watui wote.”
Alisema serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira, imeandaa
kanuni mpya za udhibiti na usimamizi wa taka hatarishi za mwaka 2019
zilizoanza kutumika Septemba mwaka huu.
“Kanuni hizi zinasimamia taka hatarishi mbalimbali zikiwamo betri
chakavu, hivyo serikali inawahakikishia kuwa itaendelea kusimamia kanuni
hizo ipsavyo ili kudhibiti uchafuzi unaoweza kutokea na utupaji usio
salama,” alisema na kuongeza kuwa, matumizi ya niashati ya kuaminika na
endelevu hayaepukiki kwa maendeleo ya taifa na kuelekea uchumi wa
viwanda ifikapo mwaka 2025.
Simbachawene alisema: “Mafanikio katika sekta zote za uchumi, huduma
za jamii na maendeleo yanategemea upatikanaji wa kuaminika na endelevu
wa nishati ya kutosha usiokuwa na madhara katika mazingira.”
Alisema
sekta ya viwanda kutumia fursa hiyo kujipatia umeme katika vyanzo vya
nishati safi na nafuu kwa shughuli za viwanda kwa mifumo na kazi kama
kuchemsha mahji, kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji na majiko sanifu
kwa taasisi za umama kama shule na majeshi.
“Natoa mwito kwa taasisi za umma kama majeshi, magereza,
hospitali, shule na vyuo kuingia katika matumizi ya teknolojia ya
nishati jadidifu maana miti mingi inakatwa na magereza na shule hivyo,
uharibifu wa mazingira ni mkubwa,” alisema
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Jeroen Verheul alisema ili
teknolojia ya nishati jadidifu isambae na kutumika zaidi kwa umma,
lazima kuwepo mazingira rafiki zaidi ya kisera na kisheria na kwamba,
sula hjili linahitahji ubia wa dhati.
Alisema nchi yake itaendelea kushitrikiana na Tanzania katika
kusaidia matumizi ya teknolojia ya nishati jadidifu am,bayo ni msaada
katika mapambano ya kidunia dhidi ya majanga yatokanayo na mabadiliko ya
tabia nchi.
Awali, Mhandisi Magali ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TAREA na
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonesho hayo, alimwambia waziri
kuwa, licha ya TAREA na wadau mbalimbali kuhamisisha matuimizi
yteknolojia ya nishati jadidifu, zipo changamoto kubwa za kudhibiti taka
zitokanazo na bidhaa za kielektrponiki zikiwamo runinga na friji.
“Taka za kielektroniki zimeendelea kuongezeka na tupo kwenye hatari
kubwa ya uchafuzi wa mazingira kupitia taka hizi,” alisema magali.
Akaongeza: “Tunaomba Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira kukamilisha
utungaji wa sheria za kusimamia biashara ya taka za kielektroniki ili
kuwezesha shughuli za urejelezaji wa taka hizo ili kuhifadhi mazingira”.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇