Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.
Jumla
ya Wasanii wapatao Saba wanaendelea na ziara yao ya kutembelea Baadhi
ya Hifadhi za Taifa hapa Nchini, lengo ikiwa ni sehemu ya kujionea
Vivutio katika Hifadhi hizo ili kuendelea kuzitangaza na kuhamasisha
wageni na wenyeji kufika Nchini kwetu kwa ajili ya kufanya Utalii.
Ziara
hiyo iliyoanzia katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato, mara baada ya
Uzinduzi wa Hifadhi za Taifa za Ibanda - Kyerwa na Rumanyika Karagwe,
ikiongozwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangala (MB),
pamoja na wasanii wa Muziki na Maigizo (Bongo Movie) ambao ni Steve
Nyerere, Dude, Richie, Shilole, Ebitoke, Shetta huku kutoka Visiwa vya
Zanzibar wakiwakilishwa na Msanii wa Muziki AT.
Wakiwa
Katika Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato, wamejionea wanyama mbali mbali
kama Twiga, Swala, Pundamilia, na Pofu, Wasanii hao baada ya kufanya
Game Drive pamoja na matembezi ya Miguu (walking safari)wamekiri
kufurahishwa na mandhali nzuri ya Hifadhi ya Burigi - Chato, kwa
kujionea uzuri wa ziwa Burigi, huduma nzuri na ukarimu kutoka kwa
wahifadhi, na zaidi huduma ya Malazi na mapumziko kwenye mahema mazuri
ya kisasa ya Mwekezaji wa kwanza katika hifadhi hiyo aitwae Wilbard
Chambulo.
Kumalizika
kwa Ziara hiyo katika Hifadhi hiyo ya Burigi - Chato, na kuelekea
katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo ambapo huko wamefanya utalii wa
kwenye Maji kwa kutembelea maeneo mbalimbali, huku wajionea Viboko,
Mamba, na Ndege wazuri wa kila aina, akiwemo Ndege aina ya Conorad
wenye uwezo wa Kusafiri kwa kuhama kwenda Ulaya na kurudi, lakini zaidi
wakipata nafasi ya kufanya Utalii wa Uvuvi (Sport Fishing).
Twiga hifadhini Burigi
Msanii
Steve Nyerere akionekana m wenye wasiwasi wakatiu wa game drive. Ni
hadi wahifadhi walipomhakikishia kwamba wanyama hawana nongwa na
binadamu ndipo akatulia...
Twiga anayepatikana ndani ya Burigi - Chato, ambae kwa mujibu wa Steve Nyerere, amedai amemsikia akiongea kingereza.... |
Pundamilia wakionekana kufurahia baada ya kuwaona (bure) wasanii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Burigi - Chato. |
Tumbili akimshangaa msanii JB
Kambi ya kitalii ya Mahema mazuri na ya kisasa ya Mwekezaji wa kwanza katika hifadhi ya Taifa ya Burigi aitwae Wilbard Chambulo.
Ndege aina ya Conorad mwenye uwezo wa kusafiri kutoka Ulaya au kwenda kulingana na msimu wa hali ya hewa, akiwa ametulia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Rubondo |
Wasanii wakiwa wameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala katika matembezi ya Kitalii (walking) Mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato |
Wasanii
wakiwa wameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi
Kigwangala katika matembezi ya Kitalii (walking) Mara baada ya kuwasili
katika hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala na wasanii wakiwa katika walking safari baada ya kuwasili katika hifadhi ya Taifa ya Burigi, Chato |
Mnyama aina ya Sitatunga kama alivyokutwa na Kamera yetu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Rubondo |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇