Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Muhimbili (MNH),Prof. Lawrence Museru (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa serikali na sekta ya afya (TUGHE),tawi la muhimbili Mziwanda Chimwege.
Na Khamisi Mussa
BAADHI ya Wakuu wa majengo (Block Managers), wakuu wa Idara na wakuu wa vitengo wamekuwa wakiwanyanyasa watumishi waliochini yao kwa kutumia vibaya mamlaka waliyopewa.
Haya yamesemwa leo Desemba 27, 2019 na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa serikali na sekta ya afya (TUGHE),tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),Mziwanda Chimwege wakati akisoma risala fupi ya mkutano mkuu wa mwaka kwa mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji Hospitali y Taita Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
Amesema changamoto kuwa kuna baadhi ya wakuu wa idara wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa watumisi waliochini yao.
Amesema changamoto nyingine ni wakuu wa idara kutotambua umuhimu wa chama cha wafanyakazi mahali pa kazi na kusababisha hamasa ndogo ya wafanyakazi hao kujiunga na TUGHE.
“TUGHE tunaona hili si sawa na si dalili njema katika kujenga taasisi yetu ili iweze kufikia matumini na mtarajiao ya Watanzania waliowengi, wanotarajia kupata huduma bora na za uhakika kutoka kwetu.Tunaomba hatua za haraka zichukuliwe ili kuthibiti hali hii,”amesema Chimwege.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa ulipaji wa posho (Allowances), mbalimbali bado haujawa mzuri kutokana na kutolipwa kwa wakati mfano malipo ya bima pamoja na malipo ya likizo.
Aidha mwenyekiti Chimwege amesema kuwa tawi hilo linawanchama 908 na kwamba wanashirikiana vizuri katika kutatua changamoto zilizopo na kuweka hali ya utulivu na amani ndani ya taasisi hiyo.
Chimwege ameushukuru uongozi wa hospitali ya Muhimbili kwa kushirikiana na tawi hilo katika masula mbalimbali yakiwamo ya vikao vinavyohusu maboresho ya posho.
Akifungua mkutano huo Prof. Museru amesema kuwa uongozi wa hospitali hiyo utaendelea kushirikiana na taasisi hiyo kwa lengo la kuleta tija katika masula mbalimbali yenye maslahi kwa wafanyakazi wake.
“Uongozi wa hoapitali ya Taifa Muhimbili haupo tayari kuona wakuu wa idara wakiwanyanyasa waliochini yao, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Pia hospitali imejitahidi kutokuweka malimbikizo kwa wafanyakazi wake, hata hivyo kuna changamoto ya rasilimali fedha kwani hazipo za kutosha,”amesema Prof. Museru.
Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa watafuatilia changamoto zinazojitokeza kwa wanachama hao wa TUGHE tawi la Muhimbili hasa kwa wasataafu kwa lengo la kupatiwa stahiki zao kwa wakati.
Akimshukuru Mkurugenzi huyo, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Tabu Mambo amesema wanajivunia kuwa na tawi la Muhimbili ambalo ni miongoni mwa tawi kubwa Tanzania nzima huku likiongoza kuwa na wanachama wengi na kwa upande wa kipato pia linaongoza.
“Tawi hili pia linaongoza kwa kuwapatia mafunzo viongozi waajiri wamatawi Tanzania nzima na hii inonyesha ile sheria ya mahusinano kazini unaitekeleza vizuri Prof.Museru,”amesema Tabu
Pia amemshukuru Mkurugenzi huyo Prof. Museru kwa kufadhili shughuli zinazofanya na TUGHE tawa la Muhimbili kwa kughramia gharama mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇