Meneja
wa kanda ya kati ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali Musa
Kazumila wakati akiongea na maofisa habari wa wizara na taasisi zake
Na.Catherine Sungura.Dodoma.
Jumla
ya sampuli 5106 zimefanyiwa uchunguzi katika maabara zikiwemo za
masuala ya kijamii na kijinai katika mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu
wa serikali kanda ya kati.
Hayo yamesemwa na
Meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Musa Kuzumila wakati wa ziara ya
maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake wakati wa kutembelea
mamlaka hiyo kujionea mafanikio yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya
afya nchini.
Kazumila amesema kwamba tangu
kuanzishwa kwa kanda hiyo miaka miwili na nusu sasa ,kanda yake
imefanikiwa kupima sampuli hizo ambazo zimefanyiwa uchunguzi katika
maabara na kuzitolea ushahidi mahakamani
"Mamlaka
ya maabara ya mkemia mkuu inasimamia sheria na kudhibiti kemikali hivyo
tumeweza kufanyia uchunguzi sampuli na hivyo kupunguzia wateja umbali
na hivyo kusaidia wananchi kupata haki na kutoa ushahidi kwa
wakati".Amesema Kazumila.
Kwa upande wa
vinasaba Kazumila amesema kati ya sampuli walizopokea jumla ya sampuli
36 zilizowasilishwa asilimia 90 zilikua zinaangalia uhalali wa baba wa
mtoto.
Hata hivyo amesema kwamba mamlaka hiyo
imeweza kukagua maeneo yanayojihusisha na kemikali zipatazo 360 pamoj na
kutoa vibali 139 za kuingiza na kusafirisha kemikali nchini kwa kanda
ya kati.
Kwa upande wa wajasiriamali wadogo
wadogo mamlaka hiyo imewapatia mafunzo wajasiriamali 315 namna ya
matumizi salama ya kemikali pamoja na kutoa elimu kwa wachenjuaji wa
dhahabu wanaotumia kemikali aina ya sodium cyanide.
Mamlaka
ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati inahudumia mikoa ya
morogoro,iringa,dodoma,singida na tabora na ilianzishwa mwaka 2017.
-Mwisho-
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇