Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa, taifa la Palestina linaupinga mpango wa Marekani wa "Muamala wa Karne" na kwamba, katu haliutambui rasmi mpango huo.
Rais Mahmoud Abbas ameashiria kusimamishwa uhusiano wa kidiplomasia wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Marekani na kueleza kwamba, madhali Rais Donadl Trump wa Marekani anaendelea kung'ang'ania maamuzi yake ya hivi karibuni kama kuhamishiwa ubalozi wa Washington mjini Baytul-Muqaddas na kuunganishwa mji wa Quds na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, mamlaka hiyo haitakuwa na uhusiano na Marekani.
Rais wa Mamlaka ya Ndani yay Palestina amesema bayana kwamba, Wapalestina wataendeleza upinzani wao dhidi ya mpango wa Marekani wa "Muamala wa Karne" na katu hawawezi kuutambua mpango huo uliojaa njama dhidi ya taifa la Palestina.
Mpango wa "Muamala wa Karne" ni mpango mpya uliopendekezwa na Marekani wenye lengo la kufutilia mbali haki za raia wa Palestina. Mpango huu umeandaliwa kwa kushirikiana na kufikiwa mapatano baadhi ya nchi za Kiarabu zikiwemo Saudi Arabia, Bahrain na Imarati.
Kwa mujibu wa mpango huo wa Marekani, Quds Tukufu itakabidhiwa kwa utawala wa Kizayuni; wakimbizi wa Kipalestina hawatakuwa na haki tena ya kurejea katika ardhi za mababu zao na Palestina itamiliki tu ardhi zitakazosalia huko katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇