LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 15, 2019

JUMAPILI LEO DESEMBA 15, 2019 KATIKA HISTORIA

  • Leo ni Jumapili tarehe 18 Mfunguo Saba Rabiuth-Thani 1441 Hijria, sawa na tarehe 15 Disemba 2019 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 839 iliyopita, alizaliwa Abul-Qasim Ja'afar Ibn Hassan Hilli, maarufu kwa jina la 'Muhaqqiq Hilli', mmoja wa wanazuoni wakubwa na faqihi wa Kiislamu, katika mji mashuhuri wa Hillah, nchini Iraq. Muhaqqiq Hilli alikuwa msomi aliyekuwa na nafasi ya juu na mtaalamu wa sheria za Kiislamu ambaye pia alibobea katika fasihi na uandishi wa mashairi. Baada ya kukamilisha masomo ya awali na kupata daraja za juu za kiroho, Muhaqqiq Hilli alitambuliwa kuwa miongoni mwa wanazuoni mashuhuri wa zama zake. Kitabu muhimu zaidi cha msomi huyo wa Kiislamu ni Sharaiul Islam fii Masaailil-Halal wal-Haraam’. Mwanazuoni huyo pia ameandika vitabu vya “Nafi', 'Maarij' na Tanbih”. Muhaqqiq al Hilli alifariki dunia mwaka 676 Hijria akiwa na umri wa miaka 74.
Ayatullah Abul-Qasim Ja'afar Ibn Hassan Hilli
Katika siku kama ya leo miaka 187 iliyopita alizaliwa Alexandre Gustave Eiffel mhandisi na msanifu wa mnara mashuhuri wa Eiffel. Umashuhuri wa Alexandre Gustave unatokana zaidi na usanifu na uhandisi wake wa mnara wa Eiffel mjini Paris ulioanza kujengwa tarehe Mosi Julai 1887 chini ya usimamizi wake. Mnara wa Eiffel una urefu wa mita 324 ambapo katika zama zake ulikuwa mnara mrefu zaidi duniani. Alexandre Gustave Eiffel aliaga dunia tarehe 27 Desemba 1923 akiwa na umri wa miaka 91.
Alexandre Gustave Eiffel
Siku kama ya leo miaka 167 iliyopita alizaliwa mwanafikizia wa Kifaransa Henri Becquerel. Becquerel ambaye aliyevumbua mnunurisho au miale ya Radioactive baada ya kufanya utafiti katika mada za urani na vitu vinginevyo, alianza kufanya jitihada za kupata vitu vinavyotoa miale ya X baada ya miale hiyo kugunduliwa na mwanafizikia wa Kijerumani, Wilhelm Conrad Röntgen tarehe 8 November 1895. Mwaka 1896 Becquerel aligundua mnunurisho  unaoweza kuzalisha miale ya X. Utafiti wa mwanafikizia huyo wa Kifaransa ulimfanya atunukiwe tuzo ya Nobel mwaka 1903. Msomi huyo alifariki dunia mwaka 1908.
Henri Becquerel
Siku kama ya leo miaka 86 iliyopita alifariki dunia mjini Najaf, Iraq na akiwa na umri wa miaka 68 Ayatullah Mirza 'Ali Shirazi' mmoja wa maulama wakubwa wa ulimwengu wa Kiislamu. Ayatullah Ali Shirazi alisoma elimu ya fiqhi na elimu nyingine za Kiislamu kwa maulama wakubwa kama vile Ayatullah Fishariki Isfahani na Ayatullah Mirza Muhaqqiq Shirazi, ambapo akiwa na umri wa miaka 22 alifikia daraja ya ijtihadi. Aidha mbali na Ayatullah Mirza 'Ali Shirazi' kutabahari katika elimu ya fiqhi na usulufiqhi, pia alibobea katika elimu ya theolojia, tiba, falsafa, historia na fasihi. Aidha kwa muda fulani alikuwa marjaa taqlidi wa Waislamu.
Ayatullah Mirza 'Ali Shirazi'
Siku kama ya leo miaka 69 iliyopita, yaani sawa na tarehe 24 Azar 1329 Hijiria Shamsia, alifariki dunia Hujjatul Islam Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani. Msomi na alimu huyo wa Kiirani aliyekuwa mmoja wa watoa waadhi na makhatibu mashuhuri katika zama zake alikuwa na azma na irada imara ya kueneza na kuwafikishia walimwengu maarifa ya Uislamu na ya Ahlul-Beit (as). Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani alikuwa akitoa mihadhara mjini Mash'had Iran na katika miji mingine na kadhalika katika Haram ya Imam Hussein (as) katika mji wa Karbala na Haram ya Imam Ali bin Abi Twalib (as) huko Najaf, Iraq. Hatimaye akiwa na umri wa takribani miaka 82 aliaga dunia katika siku kama ya leo na kuzikwa katika Haram ya Imam Ali bin Mussa al-Ridha (as) mjini Mash'had.
Hujjatul Islam Sheikh Mahdi Waidhi Khorasani
Siku kama ya leo miaka 63 iliyopita, alifariki dunia Walt Disney shakhsia mashuhuri wa sekta ya filamu za watoto. Disney alizaliwa mwaka 1901 huko Marekani. Walt Disney alihitimu masomo yake katika Chuo Kikuu cha Havard na kutunukiwa shahada ya uzamifu katika taaluma ya uchoraji na uchongaji (Fine Art). Disney alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha sanaa ya filamu za katuni. Mara kadhaa alitunukiwa tuzo za Oscar katika uwanja huo wa kutengeneza filamu za katuni.
Walt Disney
Na siku kama ya leo miaka 44 iliyopita, yaani sawa na tarehe 15 Disemba 1975, zilimalizika zama za udhibiti na ushawishi wa Uhispania huko Sahara ya Magharibi baada ya nchi hiyo kulazimika kuondoka katika eneo hilo. Polisario ni moja ya harakati za ukombozi wa Sahara Magharibi zilizowalazimisha Wahispania kukimbia eneo hilo. Harakati hiyo iliundwa mwaka 1973 baada ya wanamapinduzi wa Sahara kuasisi makundi kadhaa ya kupigania ukombozi wa eneo hilo.
Bendera ya eneo la Polisario

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages