Mshindi
wa jumla wa mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019 Victor Joseph
kutoka klabu ya Gymkhana mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje Mh Dumbaro katika mashindano yaliyomlizika
katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha jana.
Mshindi
wa Mikwaju ya jumla wa mashindano ya gofu ya Tanzania Open 2019, M
Chadha kutoka klabu ya Kili akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi
kutoka kampuni ya Oryx Energy, Sira Muhele katika mashindano
yaliyomalizika katika Uwanja wa Kili Jijini Arusha jana.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Damas Ndumbaro
amehitimisha Mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania Open jijini Arusha
huku mcheza gofu Victor Joseph kutoka klabu ya Gymkhana ya Dar es
Salaam akitwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Mchezaji
huyo kutoka Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana alifanikiwa kubakiza kombe
baada ya kuibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyoshirikisha wachezaji
toka Nchi Sita kwa kupata Mikwaju (Gross) 294.
Siku
ya kwanza Mchezaji huyo alicheza 75,74,71 na 74 akifuatiwa Joseph
Chinywai kutoka Uganda aliyepata mikwaju 308 na kuwashinda wachezaji
wengine wa divisheni A walioshiriki mashindano hayo.
Katika
Mikwaju ya jumla Net Manraj Chadha wa kili golf aliibuka na Ushindi
baada ya kupata Mikwaju ya Jumla 291 huku akiwa amecheza 72,74,71 na 74
katika mzunguko wa Mwisho.
Mshindi
katika Divisheni B ni Joe Lee ambaye alipata mikwaju ya jumla 149
baada ya kucheza 71 na 78 katika mzunguko wa pili huku kiwango chake
cha makosa kikiwa ni 18.
Mshindi
katika kundi la senior ni Boniface Nyiti wa Lugalo aliyepiga Mikwaju
yaa Jumla 162 baada yaa mzunguko wa kwanza kupata mikwaju 81 sawa na
mzunguko wa pili huku kiwango cha makosa kikiwa ni Nane.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mwenyekiti wa TGU Criss Martin
alisema mashindano haya ni mashindano ya 69 tangu kuanzishwa kwake
lakini kumekuwa na Changamoto nyingi na kuomba Rais Magufuli kutupia
Jicho mchezo huo.
“
tunatambua kazi kubwa ya Mh Rais katika Majukumu mbalimbali ambayo
amekuwa akifanya lakini tunaomba atupie jicho pia Mchezo huu umekuwa na
mafanikio” Alisema Mwenyekiti.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Ndumbaro aliahidi kufikisha kilio chao kwa
wahusika ili kuendeleza mchezo huu nap engine kwa kuanzia ngazi yaa
Mashuleni ili kupata vipaji na kuzalisha wachezaji bora wakiwemo wa
kulipwa
“
Nitafikisha Kilio chenu Serikali ili kuboresha Mchezo huu lakini pia
hakikisheni mnasajili viwanja ili viwango vya Uchezaji viweze
kutambulika Kimataifa “. Alisema Naibu Waziri Ndumbalo
Aidha
alisema Mashindano yamefanikiwa na hiyo ni kutokana na Kazi nzuri
waliyofanya kwa kushirikiana na na kamati ,waratibu Verge Africa na
wadhamini ambaao wamefanya Zawadi kuwa Bora hivyo inahitaji kuendelezwa.
Klabu
za Tanzania zilzoshiriki mashindano haya yaliyodhaminiwa na Oryx, Super
Doll, Garda word, Coca Cola, Tanfoam, Hal na Serengeti ni Lugalo, Dar es
Salaam Gymkhana zote za Dar es Salaam, Morogoro Gymkhana, Arusha
Gymkhana, TPC, Moshi na Zanzibar Sea Cliff .
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇