Mbunge wa Buchosa Mhe.Charles Tizeba akiongea na wananchi wa kisiwa
cha Kome, wakati wa ziara ya Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu (hayupo
kwenye picha) katika kisiwa hicho.
Wananchi waliofika kwenye mkutano, kumsikiliza Waziri wa Afya Mhe Ummy
Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Kisiwa cha Kome Jijini Mwanza.
Kitanda cha upasuaji pamoja na mashine yake kilicho katika kituo cha Afya Kome, katika Kisiwa cha Kome Jijini Mwanza, ambacho kitawasaidia akina mama wajawazito wanapopata uzazi pingamizi.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwasalimia wananchi wa kisiwa cha Kome baada ya Mkutano wa kuwasikiliza kero zao kumalizika.
Waziri Ummy Mwalimu akimjulia hali Bi. Ester Juma, mzazi aliyejifungua katika kituo cha Afya Kome, kisiwa cha Kome kilichopo Mkoa wa Mwanza.
Waziri Ummy Mwalimu akimjulia hali Bi Adela Deus aliyekuwa akipokea huduma baada ya kujifungua katika kituo cha Afya Kome.
Waziri wa Afya Mhe.@umwalimu Ummy akikabidhi moja ya vitanda kumi na moja vya wagonjwa vilivyonunuliwa na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Charles Tizeba.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wananchi waliofika kwenye mkutano, wakati alipofanya ziara katika Kisiwa cha Kome Jijini Mwanza. |
Kitanda cha upasuaji pamoja na mashine yake kilicho katika kituo cha Afya Kome, katika Kisiwa cha Kome Jijini Mwanza, ambacho kitawasaidia akina mama wajawazito wanapopata uzazi pingamizi.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiwasalimia wananchi wa kisiwa cha Kome baada ya Mkutano wa kuwasikiliza kero zao kumalizika.
Waziri Ummy Mwalimu akimjulia hali Bi. Ester Juma, mzazi aliyejifungua katika kituo cha Afya Kome, kisiwa cha Kome kilichopo Mkoa wa Mwanza.
Waziri Ummy Mwalimu akimjulia hali Bi Adela Deus aliyekuwa akipokea huduma baada ya kujifungua katika kituo cha Afya Kome.
Waziri wa Afya Mhe.@umwalimu Ummy akikabidhi moja ya vitanda kumi na moja vya wagonjwa vilivyonunuliwa na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Charles Tizeba.
Na.Catherine Sungura,Buchosa
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
ameahidi kuwapatia mashine ya x-ray ya kisasa ya kidigitali kituo cha
afya kome kilichopo halmashauri ya Buchosha wilayani Sengerema.
Waziri Ummy ametoa ahadi hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi kisiwani hapo ya kujionea hali ya utoaji huduma za afya.
“Ninawaahidi
wananchi nitaleta x-ray mashine ya kidigitali kwenye kituoa hichi cha
afya ili msivuke maji kwenda kupata huduma za vipimo wilayani
sengerema".Alisema Waziri Ummy
Aidha,
alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosha Crispian Luanda pamoja
na Mganga Mkuu wake Dkt. Ernest Chacha kwa jitihada kubwa wanazofanya
za kuboresha huduma za afya kwenye halmashauri hiyo"Nimefurahi kumuona
daktari wa upasuaji kwenye kituo hiki na hongereni kwa kumpatia mafunzo
ya mwaka mzima kwenye eneo hili,sasa mnatakiwa kuweka vifaa na huduma za
mtoto njiti ili kusiwepo na vifo vya watoto hao endapo itatokea".
Hata
hivyo Waziri Ummy aliwataka akina mama wa kisiwa hicho kuhudhuria
kliniki mara nne mara wanapokuwa wajawazito ili kuepukana na vifo vya
wajawazito na watoto pamoja na kuepusha kuzaa watoto walemavu.
"Tumeanzisha
huduma za upasuaji kwenye kitua hiki cha afya tunataka mama mjamzito wa
Kome akipata tatizo la mtoto kukaa vibaya tumboni au mama akipata kifaa
cha mimba asaidiwe hapa hapa"Alisisitiza Waziri Ummy.
Naye
Mbunge wa Buchosa Dkt. Charles Tizeba ameishukuru Serikali kupitia
Wizara ya Afya kuwajengea jengo la upasuaji pamoja na vifaa hivyo
kuondoa tatizo kubwa la upasuaji lililokuwa linawakabili wananchi wa
Kome na kuomba wizara kuwapatia vifaa vya vipimo katika vituo vya huduma
za afya kwenye halmashauri hiyo kwani wananchi wameanzisha ujenzi wa
zahanati 30 kwa nguvu zao hivyo wakikamilisha miundombinu huduma za afya
zitakuwa zimeboreshwa kwenye jimbo lake.
Kisiwa
cha Kome kimeongeza idadi ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo
vya huduma za afya kutoka asilimia 42 mwaka 2015 kati ya akina mama 100
hadi kufikia asilimia 80 kwa mwaka ambapo wastani wa akina mama 50
wanajifungua kwa mwezi.
-Mwisho-
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇