Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, anayetambuliwa na kanisa hilo kwa jina la Baba wa Uzao, akiongoza ibada iliyobeba mada kuu ya 'Afrika siyo giza ni Nuru', iliyofanyika leo katika ukumbi wa Namanga Star Hall, katika mji mdogo wa Namanga mkoani Arusha. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
CCM Blog, NAMANGA
Imeelezwa kwamba Rais Dk. John Magufuli amepata mafanikio makubwa katika utendaji wa kazi zake kwa sababu anayaishi anayoyaahidi kutokana na kuongozwa na utendaji wa moyo badala ya nafsi.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa 'Kanisa Halisi la Mungu Baba', anayetambuliwa na kanisa hilo kwa jina la Baba wa Uzao, wakati akiongoza ibada iliyobeba mada kuu ya 'Afrika siyo giza; ni Nuru', iliyofanyika leo katika ukumbi wa Namanga Star Hall, katika mji mdogo wa Namanga mkoani Arusha.
"Na ushuhuda ninao, Rais Dk. Magufuli ni miongoni mwa watu wanaoishi katika dhamira ya kuongozwa na utendaji wa moyo na kinachofanya yule Mheshimiwa Magufuli afanikiwe tangu alipoinuliwa kuwa rais ni kwamba anaishi kwa utendaji wa moyo siyo nafsi", alisema Kiongozi huyo wa Kanisa hilo na kuongeza;
"Mnakumbuka ahadi alizozitoa wakati anagombea kuwa Rais na pia hotuba yake aliyoitoa Bungeni alipoinuliwa kuwa Rais ni kuwa aliahidi mambo mengi ya kuiboresha Tanzania na hadi sasa karibu yote aliyoahidi ameyatekeleza, ndiyo maana tunasema yeye ni nuru kama ilivyoandikwa katika Biblia",
"Kama mnasema mimi muongo, hivi karibuni kuna waliompa PhD kwa ajili ya kuwa na sifa hiyo, sasa na wenyewe mtasema ni waongo? Je, mnawajua? Waliompa Php ni Dodoma University (Chuo Kikuu cha Dodoma).
Walimpa PhD hiyo kwa kuwa waliona na kukubali kuwa anaishi moyo wake, yaani akiahidi anatenda, sasa kuanzia leo kila mmoja lazima aishi hivyo", alisema Kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, huku zikihanikiza sauti za waumini wakisema ' Imekuwaaa', neno ambalo ni kaulimbiu ya Kanisa hilo katika kumtukuza Mungu.
Kiongozi huyo alisema, inawapasa binadamu sasa kuishi katika yale wanayosema au kuahidi mioyoni mwao kwa kuwa kwa mujibu wa Kanisa hilo utendaji wa nafsi uliokuwa unasababisha watu waibiane vipawa, karama, viwekezo na taranta ulishafikia kikomo.
Aliongeza kufafanua katika mahubiri yake kuwa kuishi moyo inatakiwa yaliyoko moyoni yaonekane kwenye paji la uso, siyo kusema kwamba "usikilize maneno yangu lakini usiangalie matendo yangu",
"Tunaposema kwamba utendaji wa nafsi umekwishakoma, maana yake ni kwamba utendaji wa moyo umeanza , yaani unaishi kama unavyosema. Kuanzia sasa ile tabia ya kusema kwamba usikilize maneno yangu lakini usiangalie matendo yangu haitakuwepo tena. Hivyo kuanzia leo kila mmoja lazima aishi hivyo.", alisema kiongozi huyo.
Kwa mujibu wa Kiongozi huyo wa kanisa hilo, utendaji wa nafsi badala ya moyo ulisababishwa na miduara mikubwa mitatu ambayo iliwasumbua hata wale wote waliotumwa, Manabii Kerubi na Adamu katika Bustani ya Edeni, Nuhu wakati akitengeneza safina, Musa wakati akivusha Wana wa Esrael kutoka Misri kwenda Kaanan, hata na Yesu.
Ibada hiyo ambayo kusudi lake lilikuwa kuelimisha kuwa kwa mujibu wa maandiko ya Biblia Afrika siyo giza bali ni Nuru, ilihudhuriwa na mamia ya waumini wa dhehebu hilo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na nchi za nje ikiwemo Kenya na viongozi mbalimbali kutoka mkoa wa Arusha.
Your Ad Spot
Dec 7, 2019
Home
featured
Kitaifa
KANISA HALISI LA MUNGU BABA: RAIS MAGUFULI ANA UTENDAJI WA MOYO BADALA YA NAFSI
KANISA HALISI LA MUNGU BABA: RAIS MAGUFULI ANA UTENDAJI WA MOYO BADALA YA NAFSI
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About Bashir Nkoromo
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇