MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi kisutu imeuambia upande wa utetezi katika kesi ya
uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa habari za uchunguzi Erick
Kabendera kuwa waende wenyewe kwa mkurugenzi wa mashtĂ ka nchini (DPP)
ili kujua hatma ya barua ya mshtakiwa ya makubaliano ya kuomba msamaha
na kukiri kosa ( pre- baggening).
Hatua
hiyo imefikiwa wakati kesi hiyo leo Desemba 4, 2019 ilipoitwa
mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega kwa ajili ya
kutajwa na kudaiwa kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo upande wa
utetezi wakawasilisha hoja zao.
Mapema
wakili wa utetezi Jebra Kambole alidai mahakamani hapo kuwa, Oktoba 11,
2019 waliitaarifu mahakama juu mshtakiwa kuandika barua ya kuomba
msahama na kukiri kosa kwenda kwa DPP lakini mpaka leo ni miezi miwili
hawajapata mrejesho wowote kutoka kwa DPP .
"Ni
lini tutakamilisha mchakato wa majadiliano hayo kwani mpaka sasa hakuna
chochote ambacho kimefanyika na mtuhumiwa bado yuko gerezani na ni
mgonjwa", ameuliza Kambole
Akijibu
hoja hizo wakili wa serikali Easter Martin amekiri kwamba ni kweli
maombi yao hayo yapo kwa DPP toka Oktoba 11 hadi leo lakini suala la
makubaliano si maamuzi yanayoweza kutolewa mara moja, ni vema waende
katika ofisi ya DPP ili wajue kinachoendela.
Hakimu
Mtega nae amesema, kufuatia hoja hizo, amewataka upande wa utetezi
waende wenyewe kufuatilia jalada la kesi kwa DPP ili wajue
kinachoendelea na ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena Desemba
18, mwaka huu.
Katika
kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye
mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh milioni 173.
Katika
mashtaka ya kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera
alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la
uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.
Inadaiwa
kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh
173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia
inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo
ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.
Mwimsamaha na kukiri kosa ( pre- baggening).
Hatua
hiyo imefikiwa wakati kesi hiyo leo Desemba 4,2019 ilipoitwa mahakamani
hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janet Mtega kwa ajili ya kutajwa na
kudaiwa kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo upande wa utetezi
wakawasilisha hoja zao.
Mapema
wakili wa utetezi Jebra Kambole alidai mahakamani hapo kuwa, Oktoba
11,2019 waliitaarifu mahakama juu mshtakiwa kuandika barua ya kuomba
msahama na kukiri kosa kwenda kwa DPP lakini mpaka leo ni miezi miwili
hawajapata mrejesho wowote kutoka kwa DPP .
"Ni
lini tutakamilisha mchakato wa majadiliano hayo kwani mpaka sasa hakuna
chochote ambacho kimefanyika na mtuhumiwa bado yuko gerezani na ni
mgonjwa", ameuliza Kambole
Akijibu
hoja hizo wakili wa serikali Easter Martin amekiri kwamba ni kweli
maombi yao hayo yapo kwa DPP toka Oktoba 11 hadi leo lakini suala la
makubaliano si maamuzi yanayoweza kutolewa mara moja, ni vema waende
katika ofisi ya DPP ili wajue kinachoendela.
Hakimu
Mtega nae amesema, kufuatia hoja hizo, amewataka upande wa utetezi
waende wenyewe kufuatilia jalada la kesi kwa DPP ili wajue
kinachoendelea na ameiahirisha kesi hiyo hadi itakapotajwa tena Desemba
18, mwaka huu.
Katika
kesi hiyo, Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye
mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa Sh milioni 173.
Katika
mashtaka ya kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera
alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la
uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.
Inadaiwa
kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya Sh
173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Pia
inadaiwa Kabendera alitakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo
ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji kodi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇