LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 4, 2019

HUMPHREY POLEPOLE AZUNGUMZA JAMBO BAADA YA SUMAYE KUONDOKA CHADEMA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amemwambia Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye kuwa alimueleza asingeweza kupata kazi ya kushauri chama chochote cha siasa kama angekuwa nje ya Chama Cha Mapinduzi.

Polepole ametoa kauli hiyo kupitia mtandao, saa chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye kutangaza kujiondoa ndani ya CHADEMA kwa kile alichokidai kuwa hakuna demokrasia ya kweli.

Polepole ameandika; Mzee nilikwambia, kazi ya ushauri hutaipata ukiwa nje ya CCM wenzako wanaotushauri na tunazingatia ushauri wao kwasababu tunawaheshimu, ni wana CCM na kiitikadi tuko pamoja. Sasa umebaki bila Itikadi. Ile ni mali ya Mtu ni yake, nilikwambia mwache, ona sasa unahama mara ya pili

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages