Na Lydia Lugakila, Kagera
Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Dkt Bashiru Ally ameagiza kufukuzwa kwa wanachama wenye mienendo mibovu yenye kukwamisha umoja
ndani ya chama hicho wakiwemo wenye fitina, kuvujisha siri za chama na kuwataja kama wadhoofishaji wa kubwa wa chama hicho.
Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally ametoa kauli hiyo wakati akiongea na
viongozi wa chama hicho katika ukumbi wa ofisi za chama zilizopo manispaa ya Bukoba mkoani Kagera .
Dkt. Bashiru amesema umoja kwa wanachama wa chama cha mapinduzi ni wa lazima wala si wa hiari hivyo ameagiza viongozi watendaji wakuu ndani ya chama hicho kuwafukuza Mara moja wanachama ambao wanakidhoofisha chama.
Amesema tatizo kubwa lipo kwa viongozi wa chama na jumuhiya zake waliopewa dhamana ya kuimalisha umoja ndani ya chama hao ndo wana kuwa chanzo cha kudhoofisha chama.
"eneo moja ambalo hutugonganisha sana ni msimu wa uchaguzi vikao vya uteuzi vinajigeuza vyenywe
kama vile ndo vyenye, wanachama wanasahau kabisa kwamba wamepewa dhamana ya kusimamia haki za wanachama, sasa nasema wenye vitendo vya namna hiyo ikiwemo fitina , kuondoa amani ndani ya chama, uvujishaji siri na upotoshaji hao wote ondoa Mara moja" alisema Katibu huyo.
Akizungumzia vitendo vya uvujishaji siri ndani ya chama hicho amesema katika uchaguzi uliopita wanachama walivujisha siri za vikao na watu wakapata nafasi ya kufanya mbinu zao kutokana na uvijishaji wa siri za chama jambo lilisababisha kuodoa adhi ya vikao vya chama.
"Sasa kwa tathimini watafuteni wale wote waliovijisha siri wachukuliwe hatua za kisheria kwa mujibu wa kanuni" alisema katibu huyo.
Amesema vikao vya chama havifanyiki mitandaoni, wala
kwenye simu na maamuzi ya chama ni maamuzi ya vikao vya pamoja kwa heshima ya chama
Ameongeza kuwa ni mwiko kwa kiongozi wa chama anayeshiriki kufanya maamuzi kwenye vikao
kuvujisha siri na kueleza namna hatua zilivyochukuliwa kwa watu ambao hawahusiki na vikao
vile.
Dkt Ally amekemea pia baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaoshambuliana kupitia mitandao ya kijamii kuwa huo ni udhalilishaji wa viongozi wenyewe pamoja na kukidhoofisha chama.
Katibu huyo ameongeza kuwa chama hicho hakiko tayari kuendana na wanachama wenye mazoea ya kizamani, wanaopokea Rushwa, wabaguzi, na kutaka tathimini ifanyika kwa ngazi ya kata, wilaya na mkoa ili viongozi hao waondolewe kwa haraka.
Kwa upande wake katibu mwenezi mkoa wa Kagera
Hamimu Muhamud amemshukuru katibu mkuu huyo na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo hayo na
kuendelea kuimalisha misingi bora ndani ya chama hicho.
Hata hivyo Katibu Mwenezi wa Mkoa huo Muhamud Ameongeza kuwa atahakikisha viongozi wa chama hicho wanasimamia haki kikamilifu.
Your Ad Spot
Dec 28, 2019
DK. BASHIRU ALLY: WANACHAMA WENYE MIENENDO HII WAFUKUZWE
Tags
featured#
habari picha#
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
habari picha
Tags
featured,
habari picha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇