Balozi
wa Tanzania nchini Uganda, Dkt. Aziz Ponary Mlima akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Chama cha wanafunzi wa Kiswahili Vyuo Vikuu Afrika
Mashariki (CHAWAKAMA), uliofanyika jana tarehe 30 Novemba 2019, katika
Chuo Kikuu Cha Ndejje, kilichopo Luwero nchini Uganda.
Tukio
hilo lilihudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria wa Uganda, Jenerali
Kahinda Otafiire, Jenerali Salim Saleh, Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo Prof.
Semakula Kiwanuka, Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Eriabu Lugujjo. Zoezi hilo
pia lilihudhuriwa na Prof Aldin Mutembei kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es
Salaam.
Katika
hotuba ya aliyoitoa Balozi Aziz P. Mlima, alizungumzia mchango wa
Mwalimu Julius Nyerere kwa harakati za ukombozi wa Afrika kusini na
Uganda na mchango wa Kiswahili kwa umoja wa kitaifa.
Prof.
Aldin Mutembei alizingumzia maendeleo ya lugha ya Kiswahili kama moja ya
lugha adhimu katika umoja wa nchi za kiafrika na jinsi kiswahili
kinavyoweza kutumika bila kudhoofisha lugha zingine za kiasili.
Jenerali Kahinda Otafiire alimwakilisha Rais Yoweri Museveni kwenye mdahalo huo.
Wanafunzi na uongozi wa Chawakama kutoka Chuo Kikuu cha Makerere walishiriki katika uzinduzi na mdahalo huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇