NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
KATIBU
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza,Salum Kalli, amesema CCM
wanaodhani itaondoka madarakani wamechelewa bali itaendelea kuongoza
nchi kutokana na misingi yake na kukubalika kwa wananchi.
Alisema
vipo vyama barani Afrika vilianguka na kuondoka madarakani sababu ya
viongozi wake kushindwa kusimamia misingi lakini si kwa CCM.
Kalli
alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari
ya Wasichana Bwiru jana kuwa, CCM itendelea kuongoza na kushika kwa
miaka 100 kutokana na uimara wa misingi yake na jinsi inavyokubalika kwa
wananchi.
“Zipo
nchi zinaongozwa kifalme,kidini na kisiasa.Tanzania inaongozwa kisiasa
chini ya Chama Cha Mapinduzi , hivyo kitendelea kuongoza kwa muda mrefu
kutokana nakutekeleza mmbo mengi ya kijamii, wenye ndoto kuwa kitaondoka
madarakaniwamechelewa sana,”alisema.
Katibu
wa CCM mkoani humu alisema tangu nchi ipate Uhuru mwaka 1961 ni mengi
yamefanywa katika sekta mbalimbali ukiwemo ujenzi wa shule, hospitali,
vituo vyaafya na zahanati, reli,miundombinu ya barabara na maji, yote
hayo si miujiza nikazi ya CCM.
Alisema
wakati nchi inapata Uhuru akina mama walijifungulia vichakani, kulikuwa
na shule 22 za sekondari lakini leo kila kata ina shule ya sekondari na
nyingine zaidi yamoja na akina mama wanajifungulia vituo vya afya na
hospitali.
Kallia
alifafanua kuwa Mwalimu Nyerere aliweka misingi ya usimamizi wa elimu
wakiwemo viongozi wengine waliofuata baada yake na sasa Rais John
Magufuli anatoa elimubure huku wazazi wakibaki kuangalia mahitaji
mengine ya watoto, malezi na nidhamu.
“RaisMagufuli
amenunua ndege lakini wapo wanaopinga hazina maana, si lazima tuzipande
wote la hasha.Wataokazipanda watalipa nauli na serikali itaongeza shule
nyingine na kutoa huduma zingine kwa wananchi,”alisema Kalli.
Alielea
kuwa elimu wanayoitafuta itawapa heshima wanafunzi haona hivyo hawana
budi kujibibidisha kwenye masomo ili wapatikane wana sayansi wakumrithi
Rais Magufuli, maprofesa,madaktari na watalaamu wa kada zingine lakini
pia wajenge uzalendo kwa nchi yao kabla na baada ya masomo .
Aidha,Kalli
ambaye alikuwa shuleni hapo kushiriki na wanafunzi wa klabu ya Jogging
kufanya mazoezi ya kujenga mwili alitumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi
hao pamoja na jamii kufanya mazoezi yakuimarisha miili yao na kujenga
afya ili kuepukana na maradhi.sss
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇