Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia)
akimuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw.
Cheptoo Amos Kipronoh (hayupo pichani) kuweka katika vipaumbele vya
Benki hiyo kwa Tanzania kuhusu ujenzi wa Barabara ya Morogoro Dodoma
yenye upana wa njia nne, kulia ni Kamishna Msaidizi wa Bajeti Bw.
Emmanuel Tutuba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Cheptoo Amos
Kipronoh, akieleza nia ya Benki yake ya kusaidia miradi mbalimbali ya
maendeleo ukiwemo ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato Jijini Dodoma,
wakati wa Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Amos
Cheptoo, baada ya mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo,
Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kulia),
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Amos
Cheptoo, (wa nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa
waandamizi wa Wizara hiyo na Benki ya AfDB , Jijini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Amos Cheptoo,
wakiwa katika Mkutano Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
WAZIRI
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameiomba Benki ya Maendeleo ya
Afrika kuipatia Tanzania mkopo nafuu kwa ajii ya kujenga barabara ya
njia Nne kuanzia Morogoro hadi Dodoma ili kuboresha usafiri na
usafirishaji wa abiria na mizigo
Dkt.
Mpango ametoa ombi hili Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo
na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo
anayewakilisha nchi nane za ukanda wa Afrika Mashariki Bw. Amos Cheptoo.
“Barabara
hii ilijengwa muda mrefu miaka ya 80, malori mengi yanapita hapa kwenda
Mwanza, Kigoma na nje ya nchi ikiwemo Burundi, Rwanda, na unaona kabisa
imeelemewa na imeanza kuharibika” Alisema Dkt. Mpango
Alisema
amemwomba Mkurugenzi Mtendaji huyo wa AfDB waanze kuliweka jambo hili
kwenye miradi itakayogharimiwa na Benki hiyo baadae ili barabara hiyo
itakayo kuwa na uwezo wa kuelekeza magari mawili kwenda upande mmoja na
mengine mawili kupita upande mwingine iweze kujengwa.
“Baada
ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi, tunahitaji usafirishaji kwa njia ya
barabara uwe na tija zaidi, uende haraka zaidi lakini pia kupunguza
ajali. Hivi sasa kuna ajali nyingi sana kwa sababu magari yanayokwenda
Dar es Salaam na yanayokuja Dodoma au kwenda Mwanza yanapishana kwenye
haka kanjia kamoja” alisisitiza Dkt. Mpango
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya
Maendeleo ya Afrika Bw. Amos Cheptoo aliyeko nchini kwa ziara ya kikazi
ya siku mbili, alisema Benki yake itahakikisha Tanzania inapata mikopo
ya miradi yake ya kimkakati na ya kipaumbele ukiwemo huo wa barabara ya
Morogoro hadi Dodoma.
Katika
hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika- AfDB, Bw. Cheptoo Amos Kipronoh, ameitaka Sekta
Binafsi nchini Tanzania kuchangamkia fursa za mikopo nafuu zilizopo
katika Benki hiyo.
Bw.
Kipronoh alisema kuwa Sekta Binafsi nchini Tanzania ina nafasi nzuri ya
kupata mikopo na utaalam utakaoiwezesha kujikwamua kiuchumi kwa lengo la
kutokomeza umasikini katika Bara la Afrika.
“Sekta
Binafsi hapa Tanzania haijatumia vizuri dirisha la mikopo ya Sekta hiyo
ikilinganishwa nan chi nyingine za ukanda huu wa Afrika na ninakuomba
Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango uihamasishe Sekta Binafsi ikope fedha
hizo ili kukuza mitaji yao na kuongeza tija” alisema Bw. Cheptoo
Aidha,
alisema kuwa Benki ya AfDB ipo katika hatua za mwisho za kutoa fedha
kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato Dodoma na
tayari benki hiyo imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za
mzunguko mjini Dodoma pamoja na miradi mipya ya kuzalisha Nishati ya
umeme ambayo iko mbioni kuwasilishwa katika vikao vya Bodi ya Benki hiyo
hivi karibuni.
Mkurugenzi
huyo amempongeza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuwa kiongozi
mwenye maono ambaye amesaidia katika mabadiliko makubwa ya uchumi na
kuzitaka nchi nyingine barani Afrika kujifunza kutoka Tanzania.
“Nilipotua
nimeona jengo la abiria la III katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, daraja la juu la Mfugale na ujenzi wa Reli ya Kisasa
unaoendelea kwa kasi, miundombinu ambayo miaka miwili iliyopita
sikuikuta nilipotembelea hapa nchini” alisema Bw. Cheptoo.
Aidha,
amempongeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kwa kusimamia
na kuhakikisha uchumi unaendelea kuwa imara ikiwa ni moja ya lengo la
Benki hiyo katika jitihada za kuifanya Afrika kuwa na uchumi imara.
Kwa
upande Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amewataka
watanzania kujivunia hatua za maendeleo zinazoonekana kwa kuwa hata
wageni wanaona mabadiliko makubwa ya kiuchumi nchini.
Ameishukuru
Benki ya AfDB kwa kukubali kufadhili miradi ya barabara za mzunguko
Jijini Dodoma na pia miradi mbalimbali ya kilimo ambayo inaajiri watu
wengi, huku akibainisha kuwa kwa kipindi cha miaka minne miradi
mbalimbali imetekelezwa kwa msaada wa AfDB na kuifanya Tanzania kukua
kwa kasi kiuchumi.
Dkt.
Mpango amewataka watendaji wa Wizara yake kuhakikisha wanawakutanisha
viongozi wa Sekta Binafsi na Watendaji hao wa AfDB kabla ya kumaliza
ziara yao nchini, ili kufanya mazungumzo yatakayosaidia kutumia fursa
zilizopo katika Benki hiyo.
Aidha,
Dkt. Mpango amewataka watanzania wenye vigezo kuchangamkia nafasi
mbalimbali za kazi zinazotangazwa katika Benki hiyo ili kuongeza
uwakilishi wa wananchi hasa kutoka Afrika Mashariki, ikizingatiwa nafasi
zinazotangazwa ni za ushindani.
Benki
ya Maendeleo ya Afrika-AfDB imefadhili miradi 23 hapa nchini ikiwemo
miradi 21 ya umma na miwili ya Sekta Binafsi, katika Nyanja za Nishati,
miundombinu ya barabara, usafiri, kilimo, maji na usafi wa mazingira,
yote kwa pamoja ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 2 nuta 1
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇