Mlezi wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa
(wakwanza kulia), akiwaongoza wake za viongozi akiwemo Waziri wa
Elimu, Profesa Joyce Ndalichako (wapili kulia)wakigawa chakula kwa
wanafunzi wa shule ya Msingi Buhangija Jumuishi, Mkoani Shinyanga.
Wake
wa viongozi wakiongozwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa
(wakwanza kulia), wakigawa chakula kwa wanafunzi wa shule ya Msingi
Buhangija Jumuishi, Mkoani Shinyanga.
Mlezi
wa Kikundi cha Wake wa Viongozi cha New Millenium Women Group, Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisoma hotuba yake wakati kikundi hicho
kilipokabidhi majengo ya madarasa manne na vyoo kumi kwa Kituo cha
waototo wenye mahitaji mwalimu cha Buhangija wilayani Shinyanga Novemba
10, 2019. Kushoto ni Mgeni rasmi katika makabidhino hayo, Waziri wa
Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Umoja wa wake wa viongozi nchini Tanzania ‘Ladies of New Millenium Women Group’ umekabidhi madarasa manne yenye thamani ya shilingi milioni 65.8 na matundu 10 ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 21 yanayoendelea kujengwa katika mabweni ya shule ya Msingi Buhangija Jumuishi iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga ambayo ni maalumu kwa watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ualbino,viziwi na wasioona.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇