Wateule kwa nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali ngazi ya Kijiji ,vitongoji,Wajumbe mchanganyiko na viti maalum mwaka 2019 wa Wilaya ya Tandahimba wameapishwa leo
Akizungumza na wateule hao baada ya kuapishwa mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Benaya Kapinga aliwaeleza kuwa habari ya siasa inaishia leo kinachofuata ni kufanya kazi
"Mnatakiwa kwenda kufanya kazi katika maeneo yenu bila kujali itikadi yoyote ya vyama ,dini Wala rangi,kafanyeni kazi wananchi wanataka kuona maendeleo"alisema.
Naye mwezeshaji George Kashura aliwaeleza kuwa wananchi wanataka kujua mapato na matumizi hivyo muwashirikishe wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo
"Mfanye vikao na wananchi na msome mapato na matumizi ya fedha zinazoletwa kwa ajili ya maendeleo mbalimbali katika ngazi za vijiji na vitongoji,ili wananchi wajue kinachoendelea,"alisema Kashura
Wateule kwa nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali ngazi ya Kijiji ,vitongoji,Wajumbe mchanganyiko na viti maalum mwaka 2019 wa Wilaya ya Tandahimba wakiapishwa leo
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Benaya Kapinga akitoa neno kwa wateule
Mwezeshaji George Kashura akisistiza wateule Kusoma mapato na matumizi katika vijiji na vitongoji vyao
Hakimu Mkazi wa Wilaya Joseph Waruku akiwaapisha wateule
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇