Uzinduzi wa Kitabu na Filamu kuhusu historia ya Reli ya TAZARA umefanyika leo Beijing.
Hafla
hiyo ni sehemu ya matukio yanayoendelea ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanayofanywa na Chuo Kikuu cha Zhejiang
Normal University.
Ujenzi
wa Reli ya TAZARA ni moja ya ‘legacy’ ya Baba wa Taifa inayoenziwa
nchini China ikiwa ni alama ya urafiki kati ya China na Bara la Afrika.
Katika
hafla hiyo Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University kimetangaza
dhamira yake kuanzisha kozi ya lugha ya Kiswahili. Vilevile, wameeleza
mpango wa kuanzia kituo cha mafunzo ya uongozi kitakachojulikana kama
Julius Nyerere Study Centre.
Kituo
hicho kitashughulika na tafiti mbalimbali juu ya falsafa za Uongozi
Barani Afrika. Rais wa Zhejiang Normal University na Balozi wa Zambia
Mhe Winnie Chibesakunda, Mabalozi na Wanazuoni pia wameshiriki hafla
hii. Habari/Picha kwa hisani ya Phelista Wegessa
Balozi
wa Tanzania nchini China,Mhe.Mbelwa Kairuki akizungumza kwenye hafla
ya Uzinduzi wa Kitabu na Filamu kuhusu historia ya Reli ya TAZARA
uliofanyika jijini Beijing. Hafla hiyo ni sehemu ya matukio
yanayoendelea ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere yanayofanywa na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University.
Picha ya pamoja wakati wa uzinduzi
Wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo







No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇