Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akipeana mkono na Kamanda wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
(SACF), Ivo Ombella wakati akikabidhi gari aina ya‘Land Lover Defender’
kwa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya
ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili.
Kamanda
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella akizunguza baada ya kukabidhiwa gari
hilo.
Kamanda
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella (wa pili kulia) akiwa na maofisa wa jeshi
hilo katika hafla ya kukabidhiwa gari hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akiwa na Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa mkoa huo katika hafla ya kukabidhi gari hilo.
Gari aina ya ‘Land Lover Defender’ lililokabidhiwa kwa Jeshi la Zima moto na Uokoji mkoani hapa.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU
wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi kujiepusha na
majanga ya moto yanayotokana na uzembe au makusudi kwa kigezo cha
kutegemea uwepo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Dkt.
Nchimbi aliyasema hayo jana wakati akikabidhi gari aina ya‘Land Lover
Defender’kwa Jeshi la Zima moto na Uokoji mkoani hapa litakalotumika kwa
shughuli mbalimbali za utawala.
“Natarajia
gari hili liitasaidia kurahisisha majukumu ya kijeshi kwa Jeshi hili,
hususan kwenye eneo la utoaji elimu na kujenga maarifa kwa jamii katika
kuhakikisha suala la kinga linapewa kipaumbele ili kuepusha maafa na
ajali zozote huko mbeleni,” alisema Nchimbi.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Jeshi hilo mkoani hapa, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella, alisema gari hilo litatumika kwa
shughuli zote za dharula ndani ya jeshi hilo chini ya uratibu wa idaraya
utawala.
“Ifahamike
kuwa Jeshi la Zima moto na Uokoaji linahusika nadharula zote ikiwemo
majanga ya moto, tetemeko la ardhi, mafuriko na uzazi isipokuwa jinai
pekee,” alisema Ombella
Aidha,
aliwatahadharisha wananchi kuwa makini kwa kujiepusha na majanga ya
moto hasa nyakati za utayarishaji wa mashamba kwa kuzingatia usalama na
utunzaji mzuri wa mazingira kulingana na eneo husika.



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇