·
Washiriki wanajisajili kwa
mtandao, Tigopesa
Usajili
wa mbio za 18 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, Tigo km 21 na Grand Malt
Km 5 umeanza kwa kasi huku ukiwa juu kwa asilimia 30 ikilinganishwa na wakati
kama huu mwaka jana. Hili ni ongezeko la asilimia 10 ndani ya wiki moja.
Taarifa
iliyotolewa na waandaaji wa mbio hizo ieeleza kuwa mwendendo ni mzuri na
wamewataka washiriki kuchangamkia punguzo la bei litakalodumu hadi mwezi
Januari mwakani. Washiriki wanajisajili kwa kupitia www.kilimanjaromarathon.com na kwa
Tigopesa kwa kubonyeza *149*20#.
Mkurugenzi
wa Mbio hizo nchini, John Bayo alisema kwa kupitia taarifa hiyo kuwa kuna idadi
maalumu ya washiriki inayotakiwa kwa mbio zote tatu (Kilimanjaro Premium Lager Km
42, Tigo km 21 na Grand Malt Km 5) ili kuhakikisha kuw ambio hizo zinaendana na
viwango vya Shirikisho la Kimataifa la Riadha (IAAF) ili kuhakikisha usalama
unazingatiwa.
Kwa
mujibu wa Bw. Bayo, hii pia itahakikisha washiriki wanafurahia mbio hizo bila
ya msongamano na pia kutoa nafasi kwa waandaaji waweze kutoa huduma
zinazotakiwa katika njia ya mashindano na sehemu ya kumalizia pia.
Kuhusu punguzo la bei, waandaaji
hao pia walitoa wito kwa washiriki wachangamkie utaratibu huo ambao ulianza
Oktoba Mosi 2019 hadi Januari 14 , 2020. Kwa raia wa Tanzania na wale kutoka
nchi za Afrika Mashariki watalipa Tsh 15,000 kwa mbio za Km 42 na 21 na Tsh
5000 kwa km 5 lakini kuanzia Januari 15, 2020 hadi Februari 16, 2020 washiriki
watakaojisajili watalipa Tsh 20,000 kwa km 42 na 21 na Tsh 5000 kwa km 5.
Kwa wageni wakazi au wenye vibali
vya kuishi na kufanya kazi na wale wa nchi za SADC watalipa USD 35 kwa km 42 na
21 na USD 5 kwa km 5 kuanzia Octoba 1, 2019 hadi Januari 14, 2020 lakini
kuanzia Januari 15, 2020 hadi Februari 16, 2020 wanaojisajili watalipa USD 45
kwa km 42 na 21 na USD 5 kwa km 5.
Washiriki wa kimataifa watalipa
USD 70 kwa km 42 na 21 na USD 5 kwa km 5 kuanzia Oktoba 1, 2019 hadi Januari
14, 2020 na kuanzia Januari 15 hadi Februari 16, 2020 watalipa USD 85 kwa km 42
na Km 21 na USD 5 kwa km 5.
Kwa mujibu wa waandaaji hao,
usajili utafungwa rasmi saa sita usiku Februari 16, 2020 au pale ambapo idadi
inayotakiwa itatimia.Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka Chama Cha Riadha Tanzania, Baraza la Michezo Tanzania, Bodi ya Utalii Tannzania na wadau wengine wa riadha.
Washiriki pia walikumbushwa kuhusu vituo vya kuchukulia namba zao za ushiriki ambapo kwa Dar es Sallaam ni Mlimani City kuanzia February 22-23, 2020, Arusha ni Hoteli ya Kibo Palace kuanzia Februari 25-26 na Moshi ni Hoteli ya Keys kuanzia Februari 27-28. “Washiriki watatakiwa kujitambulisha na kuthibitisha kuwa wameshalipia kabla ya kukabidhiwa namba zao,” ilisema taarifa ya waandaaji.
Wadhamini
wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2020 ni Kilimanjaro Premium lager, Tigo, Grand
Malt Kilimanjaro Water, TPC Limited, Simba Cement, Barclays Bank na watoa huduma rasmi
ni Kibo
Palace Hotel, Keys Hotel, GardaWorld Security, Precision Air na CMC Automobiles.
Mashindano ya Kilimanjaro Marathon
yanayoandaliwa na Wild Frontiers na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive
Solutions, yanatarajiwa kufanyika Machi
1, 2020 katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Washiriki wa mbio za Tigo kilometa 21 wakianza mbio hizo Washiriki wa mbio za kilometa 42 za Kilimanjaro Premium Lager marathon wakiwa tayari kuanza mashindano hayokatika mbio zilizopita. Usajili wa mashindano hayo umeanza kwa kasi kwa njia ya mtandao na Tigopesa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇