Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,
Mhe. Amina S. Mollel Bungeni leo jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
lililohusu mpango wa Serikali wa kuwapatia huduma ya usafiri Watumishi
wa Umma wenye Ulemavu.
Happiness Shayo-Dodoma
Tarehe 14 Novemba, 2019
Serikali imezitaka Taasisi za Umma nchini kuhakikisha zinatatua changamoto yahuduma ya usafiri kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu ili wawezekutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi waUmma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kwa niaba ya Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mhe. Amina S. Mollel(Mb) (Viti Maalum) aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuwapatiahuduma ya usafiri Watumishi wa Umma wenye Ulemavu.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema kuwa, ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali,
Taasisi za Umma zinatakiwa kutekeleza miongozo inayotolewa ikiwa ni pamojana Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu wamwaka 2008 unaoelekeza Waajiri kuwapatia huduma ya usafiri au kulipiagharama za mafuta ya kwenda na kurudi kazini kwa Watumishi wa Umma wenyeUlemavu ambao wana vyombo binafsi vya usafiri, lengo likiwa ni kuwawezeshakutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, Waajiri ambao hawatekelezi Mwongozohuo, wanakiuka maelekezo ya Serikali kwa kuwanyima stahiki watumishi wenyeulemavu, hivyo wakibainika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu zakiutumishi zilizopo.
Serikali
kupitia Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini imejipanga kufanya Ufuatiliaji
wautekelezaji wa Mwongozo huo ili uweze kufanya kazi kama
ilivyokusudiwa.
Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewakumbusha Waajiri kutoa kipaumbele cha mikopoya vyombo vya usafiri kwa Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu wanaokidhivigezo vya kukopesheka ikiwa ni utekelezaji wa Waraka wa Watumishi waSerikali Na.3 wenye Kumb.Na. C/AC.7/228/01/16 wa Juni 30, 2011 unaotoaUtaratibu wa Kukopesha Fedha Taslimu Watumishi wa Serikali kwa ajili yakununulia Magari au Pikipiki pamoja na Matengenezo ya Magari na Pikipiki hizo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇