Wizara ya Afya ya Yemen jana usiku ilitoa tangazo rasmi na kusema kuwa, Wayemen wasiopungua 71 elfu wamefariki dunia baada ya kukosa matibabu kutokana na Saudi Arabia kufunga njia zote za kuingia na kutoka Yemen.
Katika tangazo lake hilo, Wizara ya Afya ya Yemen imesema, tangu Saudi Arabia na kundi lake walipoanzisha mashambulizi ya kivamizi hadi hivi sasa, wagonjwa wasiopungua 43 elfu wa Yemen wameshafariki dunia kutokana na kushindwa kwenda nje ya nchi hiyo kwa matibabu. Wagonjwa wengine 28 elfu wa magonjwa ya saratani na kensa nao wamefariki dunia kutokana na kukosa dawa na mahitaji yao ya lazima ya tiba.
Itakumbukwa kuwa tangu mwezi Machi 2015 hadi hivi sasa, Saudi Arabia imefunga njia zote za ardhini, angani na baharini nchini Yemen.
Mark Lowcock, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu hivi karibuni alisema kuwa, Yemen inakabiliwa na janga baya zaidi la kibinadamu katika historia.
Mwezi Machi 2015, Saudi Arabia kwa uungaji mkono kamili wa madola ya kibeberu kama vile Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel na kwa kushirikiana na baadhi ya tawala za Kiarabu kama vile Imarati, ilianzisha mashambulizi ya kila upande dhidi ya Yemen na kuizingira angani, ardhi na baharini nchi hiyo ya Kiarabu.
Hadi hivi sasa mashambulizi ya kikatili ya Saudi Arabia na kundi lake yameshapelekea makumi ya maelfu ya Waislamu wa Yemen kuuawa na kujeruhiwa mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.
Uvamizi huo dhidi ya nchi maskini ya Yemen umewasababishia wananchi matatizo mengine mengi kama vile upungufu mkubwa wa chakula na madawa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇