LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 24, 2019

RC MAKONDA AWAAPISHA WAJUMBE WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WILAYA YA KINONDONI NA TEMEKE

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Novemba 23, 2019 amewaapisha Wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Kinondoni na Temeke.


Walioapishwa wa Wilaya ya Kinondonu, ni pamoja na Derek Murusuri, Balozi Celestine Christopher Liundi na Mama Merina Mlunde.

Aidha RC Makonda pia aliwaapisha wajumbe wengine wane wa Wilaya ya Temeke.

 Akitoa nasaha zake baada ya zoezi hilo, Mkuu wa Mkoa Makonda aliwataka Wajumbe hao kuwa sehemu ya utatuzi wa migogoro na sio kuichochea.

Aliwataka Wajumbe hao kutumia mbinu zote kutatua migogoro ya ardhi ili mashauri yasiwe yanachukua muda mrefu.

"Muwe msaada kwa watu wote na hasa wanyonge, wajane na yatima ili wapate haki yao," alisisitiza.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akimuapisha Derek Murusuri kuwa Mjumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Wilaya ya Kinondoni. 
 RC Makonda akimkabidhi kitendea kazi Murusuri mara baada ya kumuapisha.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge (wapili kushoto), wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe hao baada ya kuwaapisha.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages