Mtoto
mmoja aliejulikana kwa jina la Mejoole Melau Loitale (14) amefariki
dunia na wengine wa tano kujeruliwa mara baada ya Radi kubwa
ilioambatana na mvua kubwa ilionyesha katika kata ya Sambaya wilayani
Arumeru.
Akiongelea
tukio hilo mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa tukio hilo
lilitokea November 23 majira ya jioni ambapo zilitokea mvua kubwa
ambazo ziliambatana na Radi ilipiga na kusababisha madhara ya watu
sita, akiwemo mtoto ambaye alifariki wakati wa jitihada za kumkimbiza
hospital zikifanyika .
Aidha
alibainisha kuwa majeruhi mmoja amelazwa katika hospitali ya Seliani
Ngaramtoni ambae ametambuliwa kwa jina la Melau likindasaru loita ( 35
)anaendelea vizuri huku majeruhi wengine wanne wameruhusiwa kurudi
nyumbani kutokana na kutopata madhara makubwa.
Muro
alitoa Rai kwa wananchi wote wa Arumeru kuendelea kuchukua tahadhari
wakati wa kipindi hiki cha mvua kikiendelea kwa kuhakikisha hawakai
chini ya miti, au kwenye nguzo za nyaya za umeme.
Alitumia
muda huo kutoa pole na rambirambi kwa familia ya Marehemu na kuendelea
kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurejea katika shughuli zao za
kawaida za kijamii.
Aliongeza
kuwa Vyombo vya ulinzi na usalama , kwa kushirikiana na vikosi vya
zimamoto na uokoaji viko katika hali ya tahadhari na utayari mkubwa wa
kukabiliana na majanga yeyote yatakayo weza kutokea hivyo aliwataka
wananchi kukaa na amani kwani Serikali ipo kwa ajili yao .
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇